Recent Comments

MBUNGE WA JIMBO LA NGARA AFANYA MKUTANO NA WASANII WA JIMBO LA NGARA,NA KUZINDUA SHIRIKISHO LAO

By Simamia Journal Feb 7, 2021

Leo tarehe 07.02.2021, MH. NDAISABA GEORGE RUHORO, Mbunge wa Jimbo la Ngara, amezungumza na wasanii wote wa Jimbo la Ngara na kuzindua Shirikisho la wasanii wote

 

Shirikisho hilo la wasanii wote wa wilaya ya Ngara linawahusisha wanamuziki mitindo mbali mbali kama vile Hip Hop,Rhumba,R&B,Singeli,Nyimbo za Injili na Sanaa ya Maigizo.

 

Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro amefanya mkutano huo kwa njia ya Mtandao (Zoom meeting) akiwa Dodoma ambako anahudhuria Vikao vya Bunge huku wasanii hao wakiwa katika Ukumbi wa Muruvyagira resort mjini Ngara

 

Mkutano huu, umefanyika kufuatia ahadi ya Mheshimiwa Mbunge aliyoitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi ambapo aliahidi kuunda shirikisho la wasanii,kuanzisha Studio ya kisasa itakayotumika kurekodi na kutayarisha Muziki wa aina zote.

 

Mheshimiwa Mbunge pia amewafahamisha wasanii hao kuwa tayari amenunua Vifaa vya Kisasa kama sehemu ya maandalizi ya kutengenezwa Studio hiyo pamoja na Vifaa vipya vya Muziki vitakavyotumika katika shughuli mbali mbali za Burudani.

 

Katika Mkutano huo,Pia Mheshimiwa Ndaisaba amesekiliza changamoto zinazowakabili wasanii hao na kuwashauri kuwa na Umoja imara ili kurahisha utatuzi wa changamoto changamoto kubwa zinazo wakabili.

 

Aidha,Kupitia Mkutano huo,Wasanii wa Ngara wamechagua Uongozi kama ifuatavyo:-

  1. Mwenyekiti Mwl. Baraka Andrea Makobwe
  2. Mwenyekiti msaidizi Mwl.Donald Elias
  3. Katibu, Isaya Cyprian
  4. Katibu Msadizi, Nuru Nzoya
  5. Mhasibu Joas Ndaba
  6. Msemaji wa ShirikishoTimothy Makobwe
  7. Promoter Denis Nyamtera

Wasanii hao pia wamemuomba Mheshimiwa Mbunge kuwa mlezi wao. Wamezitaja Changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na:-

 

Uhaba wa vifaa vya Sanaa ya maigizo,(Video Production Studio and Equipmets),Uaminifu ktika kazi,Elimu ya Muziki na Ujasiriamali,Vifaa vya hamasa,Studio ya mazoezi, pamoja na jingo maalum kama Ofisi ya wasanii,Msaada kutoka Ofisi ya Utamaduni Wilaya kwaajili ya kuwasaidia kusambaza kazi za wasanii na kuunganishwa na wasanii kutoka maeneo mengine.

 

Imetolewa na

Juventus Juvenary Ilambona

Katibu wa Mbunge

Jimbo la Ngara.

 

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv