Serikali imetoa siku 30 kwa wakurugenzi wa halmashauri sita za zilizopo katika mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanawatafuta wanafunzi zaidi 7000 waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2021 ili waweze kuendelea na masomo yao.
Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela katika kikao cha kamati ya ushauri (RCC) kilichokuwa na lengo la kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa maendeleo mkoani humo.
Alisema kuwa hadi kufikia mwezi machi mosi mwaka huu ni lazima wanafunzi wote waliochaguliwa wawe wameripotika katika shule walizopangiwa na wazazi watakaokaidi kutoa ushirikiano watachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Shinyanga ilipangiwa wa wanafunzi 26,217 kujiunga na kidato cha kwanza, lakini walioripoti shule ni 19,776, huku 7,416 bado hawajaripoti katika shule walizopangiwa,”alisema Msovela.
Aliongeza kuwa wanapaswa kushirikiana na maafisa elimu kata,watendaji wa vijiji na mitaa ili kuwabaini wanafunzi ambao bado hawajaripoti shule bila sababu za msingi.
Sambamba na hilo Msovela aliwata wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kusimamia kikamilifu zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa ili vijeyajengwe kwa kiwango bora kuendana na thamani ya fedha, pamoja kukamilika ndani ya muda uliotolewa na Waziri Mkuu ifikapo Februari 28 mwaka huu.
Awali akiwasilisha taarifa ya elimu ya mkoa kaimu afisa elimu mkoa huo James Malima alisema watahakikisha wanalitekeleza agizo hilo kikamalifu ikiwa ni pamoja na kuwachukulia htua atuki za kisheria kwa wazazi watakaobainika kufttoapeleka watototo wao shule kwa uzembe.
“Maafisa elimu kata wataputa kila kaya kufanya uhakiki ili kujua wanafunzi wambao hawajapelekwa shule,Kama wapowaliopelekwa shule za watu binafsi basi mawasiliano yatfanyika haraka Sana mpaka tuwapate wote haiwezrkakekank zaidi ya wanafunzi 7000 kutojulikana walipo,”alisema malima.
Nae mkuu wa laya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba, akimesema wao kishapu wanajipanga zaidi kujenga madarasa mengi ambapo wamejiwekea malengo ya kujenga vyumba vya madarasa 122 kwa mwaka huu pekee.
Recent Comments