Imeandikwa na Lameck Jaston,Geneva,Uswis
Nilikuwa nasikia mdau na rafiki yangu Mayweather akishauri juu ya vitambi ,vyakula ,pombe na kukaa bila mazoezi.
Nawiwa kuungana na wengi wanaopaza sauti kusema kitu juu ya lishe . Japo chakula hakiwezi kukuponya na ugonjwa, lakini kinaweza kukusaidia kukupa nguvu na virutubisho stahiki kupigana na vijidudu vinavyoshambulia mwili wako.
Ukiwa na mafuta zaidi mwilini unakuwa katika hatari ya kushambuliwa kwa kasi na magonjwa mbalimbali ikiwemo yanayohusiana na kupumua.
Binafsi sio mtaalamu wa swala la lishe lakini ninapenda kujifahamisha juu ya chakula hasa siasa Sera na diplomasia iliyo nyuma ya chakula.
Vakula vyote hatarishi kwa afya yetu lobbying/ ushawishi wake ni mkubwa mno kwa hiyo ni mhimu mtu mwenyewe kuwa makini kwa kile kinachoingia tumboni kabla ya kusubiri daktari anasema nini ,kama tunavyoambiwa tuchukue tahadhari bila kusubiri tamko.
Fikiria pesa zinazotumika kuadvertise / kutangaza vinywaji kama soda, bia na mvinyo unafikiri wasanii wakubwa na watu maarufu wanapewa Pesa ndogo kutangaza hivyo vinywaji? ukiingia bar angalia viti vyenye chapa ya âsodaâ ama bia , vibanda vya simu, internet , mpira, sherehe viti vyenye chapa hizo. Had makanisani yaan ni lobbying nzito.
Ukitaka kuthihirisha zaidi ingia supermarket yoyote angalia product/ bidhaa ( kitu chochote cha kula ) ambacho hakijaongezewa sukari kwa kusoma ingredients ( yaan unaweza kuta hata 5% ya vyakula vyote supermarket haifiki.
Kama unakunywa soda yako mara moja kwa week, au juice hizi ,bia sijui mvinyo ukaongezea na style ya maisha kutumia miguu zaidi ama baiskeli sio mbaya kabisa na hauhitaji gym.
Hatari ya chakula iko kwa kile unachokula kila siku ukiongezea na style ya kukaa sana bila kutembea kwa miguu wala baiskeli ndio tatizo zaidi. Ndio maan ni nadra kumuona mkulima, muwindaji ama mfugaji ana kitambi.
Tena kwetu Afrika tuna afadhali sana, nchi hizi za magharibi hatari ni mara 2 zaidi. Hawalimi vya kutosha, wanategemea supermarket na sera ya supermarket ni kuuza kwa wingi , wakupe radha ( kumbuka sukari ni addictive) radha inayokufanya ununue zaidi hawajali Kesho ukiumwa, ndio maana kuna hadi wataalam na wanasaikolojia wnahuska katika kupanga vitu supermarket kukamata attention yako mnunuzi.
Ushuhuda:
Binafsi nilipoamua kuwa makini na intake ya sukari, mafuta na wanga :nilikuwa naenda supermarket kununua chakula natumia zaidi ya lisaa kutafta ninachoweza kula ( fikiria supermarket yenye ghorofa kama 3 za vyakula ila unatafta chakula rafiki kwa afya yako had jasho linakutoka ( ukiacha mboga mboga na matunda)
Ni vema kuchukua tahadhari hasa ukiweza ukiwa bado kijana inakuwa rahisi kuliko umri ukishaenda utatumia nguvu zaidi ambayo wakati mwingine hauna hivyo inakuwa ngumu kidogo.
Tabia nyingine nzuri ni intermittent fasting ( mfungo wa mda Fulani/ kati) mfano kuwa na masaa 16 ukinywamaji tu bila kula( yaan kama umekula saa 2 jion usile kitu kingine hadi Kesho yake saa 6 mchana ( 16 hours) maana yake breakfast unaachana nayo unakula cha mchana na cha jion.
Hiyo faida zake ni nyingi sana kuna hata magonjwa inaua kabisa ukiacha kukata kitambi.kumbuka mwili wetu ni kama gari, kila unapokula digestion ni kama injin ya gari kwenye bara bara mbovu, inavyofanya kazi sana.Hivyo kama hauli mara kwa mara ni kama gari ambavyo huisurutishi mara kwa mara . Mwili wako unaupa pumziko.
Angalizo: huwezi fanya mfungo huo kama we ni mama mjamzito unanyonyesha ama kama mtu ana matatizo ya kiafya yasiyostahimili kukaa mda mrefu bila kula.
*Habari njema *
 Tuna bahati sana kwetu Afrika: Kula vyakula bora ni gharama ndogo zaidi kuliko vyakula visivyo bora ( ndio maana Afrika watu wenye kipato cha kati na cha juu ndio wengi wana hatari hiyo ya vitambi na sukari ukilinganisha na wenye vipato vya chini sana ).
Lakini nchi hizi nyingine za magharibi vyakula bora ni gharama kubwa sana unalipia mara mbili ya bei ya kawaida. Ndio maana nchi nyingi za ulaya na Marekani watu wenye kipato cha chini na maskini ndio wanaopata matatizo makubwa ya mafuta na sukari na vitambi kwa sababu hawawezi kumudu gharama za kula chakula bora.
Siasa nyuma ya lishe
kama dunia nzima ingehamia kwa vyakula asili visivyo na kemikali wala sukari ongezwa, Afrika tayari umaskini ungeondoka Haraka sana kwan chakula kingekuwa lulu na wakulima wetu wangeuza sana kwa bei kubwa.
Lakini tumekuwa brainwashed / kuaminishwa kula manailoni na sukari na kemikali, ili mradi tu viwanda Vikubwa vya matajiri na nchi tajiri zizidi kutengeneza pesa huku viwanda vya madawa navyo vikichungulia fursa : wakati huo huo mkulima wa chini anayezalisha chakula bora anazidi kuwa maskini na anakosa soko au anauza bei ya kutupwa. Hii ndio siasa na diplomasia nyuma ya vyakula visivyo bora.
Tutumie neema tuliyonayo kwetu kula vizuri. Nenda zaidi gengeni kuliko supermarket kama Unaweza kula zaidi vyakula vitokanavyo na mimea ni vema zaidi. Kama unaweza pata tunda kula kama lilivyo ni bora zaidi ya juice uliyokamua kwa mashine kwani process ya ukamuaji huacha fibers ambazo ni mhimu sana kwa afya wakati ukila chungwa kama chungwa au embe kama embe unapata kila kitu.
Na ukiwa na fursa jaribu âintermittent fasting ( hasa ya masaa 16) Kumbuka kufanya hayo yote ni kuinua afya yako ya familia , ya jirani na uchumi wa maskini.
Mubarikiwe sana.
Recent Comments