Baadhi ya Wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF)katika manispaa ya Shinyanga Nchini Tanzania wameeleza kubadilika kimaisha kwa kuanzisha miradi ya maendeleo,huku baadhi yao wakianza kurudiana na wenza wao baada ya kutengana kwa muda mrefu kutokana umasikini
Wananchi hao, wameiambia www.simamia.com baada ya kutembelewa na maafisa kutoka makao makuu ya Tasaf Dodoma, ambao wanapita katika kuwatembelea wanufaika mpango huo ili kujionea namna wanavyotumia fedha za ruzuku wanazopatiwa.
Magdalena Alex ni mkazi wa manispaa ya shinyanga alisema kuwa alitengana na mume wake kwa muda wa miaka 5 iliyopita baada ya hali ya umasikini kukithiri katika familia yao na kutelekezewa watoto watatu na mwenza wako.
“Mume wangu alinitoroka nyumbani na kutokomea kusiko julikana baada ya mimi kuanza kupokea fedha za ruzuku kutoka Tasaf nilijenga nyumba ya kisasa pamoja na kusomesha wanangu alirudi nyumbani na kuniomba msamaha turudiane,”alisema Alex
Alisema kuwa amelazimika kumsamehe ili waendelee kulea watoto wao kwa pamoja huku akiwaomba wanaume mkoani humo kuacha tabia ya kuwatelekeza wake zao pindi maisha yanapokuwa magumu.
.
Nae mwanaume ambaye aliikimbia familia yake ambaye hakutaka jina lake litajwe mtandaoni alisema kuwa alifanya hivyo kwa lengo la kwenda kutafuta maisha na hakuwa na nia ya kuitelekeza familia yake.
“Namshukuru mke wangu kwa kunipokea kwa mara ya pili nilimkosea lakini yeye ameamua kunisamehe,nitaendelea kumpenda na pia kuwa baba bora kwa familia yangu,”alisema mwanaume
Rejina Limi ni mkazi wa Uyogo ambaye pia ninufaika wa mradi huo alisema kuwa kabla ya kuanza kupokea ruzuku hali yake ilikuwa duni lakini kwa sasa amefanikiwa kujenga nyumba ya kisasa,kulima mahindi na mpunga.
” fedha za ruzuku ya Tasaf zimebadilisha maisha yangu na familia nzima kwa sasa nasomesha mtoto mmoja sekondari na mwingine chuo kikuu,bila msaada huu maisha yangu yangebakia kuwa duni,”alisema Limi.
Kwa upande wake mratibu wa Tasaf wa manispaa ya shinyanga Octavina kiwone alisema kuwa fedha za ruzuku wanazopatiwa walengwa kunusuru kaya masikini zimeanza kuleta matokeo chanya baada ya walengwa kujihusisha na shughuli za kiuchumi.
“Walengwa wamenunua ng’ombe,mbuzi na kuku ambazo zimewasaidia kujenga nyumba za kisasa na kuondokana na hali ya umasikini ambayo ilikuwa inawakabili hapo awali,”alisema kiwone.
Recent Comments