Salvatory Ntandu-Shinyanga
Wanafunzi 1,900 kutoka shule ya Msingi Kabale katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, mkoani Shinyanga wanakabiliwa na tatizo la uhaba vyumba vya madarasa ambapo wanalazimika kusoma kwa awamu mbili kwa siku kutoka na madarasa nane yaliyopo kutokidhi mahitaji hayo.
Kero hiyo imetolewa jana katika hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na Wadau wa elimu kampuni ya Ako group vyenye thamani ya shilingi milioni 5 katika shule hiyo iliyopo katika kata ya bulyankulu katika halmashauri hiyo kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa vyumba vipya vitatu vya madarasa ili kupunguza uhaba huo.
Kurwa Lufungulo ni mwalimu wa taaluma katika shule hiyo alisema kuwa kwa sasa wanafunzi wanalazimika kukaa darasa mmoja wakiwa zaidi 300 huku madarasa ya kwanza na lapili wakilazimika kusoma kwa awamu mbili hali ambayo imekuwa ikileta usumbufu katika hali ya usomaji.
âTatizo hili limesababishwa na ongezeko la wanafunzi kila mwaka,tunavyumba nane vya madarasa,kimoja kinatumika kama ofisi ya walimu wote wa shule hii,wanafunzi wanakaa watano katika dawati mmoja ambapo kwa sasa uwiano wa kila darasa umekuwa wanafunzi 400Â huku wengine wamekuwa wakikaa chini hali ambayo ni sio nzuri kitaaluma,âalisema Lufungulo.
Perepetua Leornadi ni mwanafunzi katika shule hiyo alisema kuwa pia wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa madawati ambapo kwa sasa wanafunzi 1900 wanakaa kwenye madawati 216 na kusababisha wanafunzi wa madarasa ya kwanza,pili na awali kukaa chini na kuiomba serikali kutatua changamoto hiyo kwa haraka ili kuboresha hali ya taaluma katika shule hiyo.
Baraka Richard ni mwanafunzi katika shule hiyo alisema kuwa wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa vyoo ambapo kwa sasa wanatuma matundu nane manne ya wavulana na manne ya wasichana ambnapo kwa sasa wanalazimika kusubiriana kwa foleni wakati wa mapumziko hali ambayo hatari kwa afya inaweza kusababisha kupata magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Ako group, Athanas Kahigi ambaye ni mdau wa elimu alisema kuwa wamelazimika kutoa vifaa vya ujenzi ambavyo ni pamoja saruji mifuko 45,nondo 35 ,mbao, mchanga lori 10Â na mawe lori 10 pamoja fedha taslimu shilingi laki sita ambazo zitatumika kumlipa fundi kwaajili ya kujenga vyumba hivyo vya madarasa na kuahidi kuendea kuichangia shule hiyo ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya serikali kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Dk Ntana kilagwire alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa kwa sasa wameunda kamati ya ujenzi mpya ambayo itasimamia ujenzi wa madarasa mapya ya shule hiyo na kuwaomba wazazi na wadau wengine wa elimu kuchangia ujenzi huo.
âMwaka huu shule hii ilikuwa isipokee wanafunzi wa darasa la kwanza, kutokana na kukosekana kwa vyumba vya madarasa tulilazimika kuivunja kamati ya shule ya awali kwa kushindwa kutimiza majukumu yao, haiwezekani wanafunzi 400 kukaa darasa mmoja wazazi wa eneo hili tuchangie ujenzi wa madarasa sisi halmshauri tutafanya ukamilishaji wa haraka,âalisema Kilagwire
Sambamba na hilo Dk Kilagwire alizitaka kampuni wa watanzani zinazotoa huduma katika mgodi wa Barrick bulyanhulu zipatazo 40Â kuiga mfano wa Ako group katika kuchangia shughuli za maendeleo katika jamii ikiwemo elimu ili kutatua kero ya uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule zinazouzunguka mgodi huo.
Mwisho.
Recent Comments