Bi Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 visiwani Zanzibar ambapo alipata elimu ya msingi kati ya 1966 na 1972  katika shule tofauti tofati katika visiwa viwili vikubwa vinavyounda Kisiwa cha Zanzibar, ambavyo ni visiwa vya Unguja na Pemba.
Samia Suluhu Hassani alianza safari yake ya elimu katika shule ya msingi Chawaka iliyopo kisiwani Unguja na baadae alihamia shule ya msingi Ziwani iliyopo kisiwani Pemba kabla ya kurejea kisiwani Unguja na kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Mahonda.
Elimu ya Upili ama Sekondari aliisoma kati ya mwaka mwaka 1973 mpaka mwaka 1976 ambapo kama ilivyokuwa kwenye elimu ya msingi,Samia Suluhu Hassan alisoma shule mbili tofauti ambapo alisoma kidato cha kwa nza mpaka cha nne katika shule ya sekondari ya Ngambo iliyopo visiwani Unguja kati ya mwaka 1973-1975 kabla ya kuhamia sekondari ya na Lumumba, iliyopo kisiwani Unguja mnamo mwaka 1976 ambapo alihitimu kidato cha nne.
Baada ya kumaliza elimu ya Sekondari,Samia Suluhu Hassan hakujinga moja kwa moja na masomo ya Chuo,kwani mwaka 1977, Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar ambapo alipanda mpaka ngazi ya kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.
Wakati akiwa mtumishi katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,Samia Suluhu Hassan alikuwa akijiendeleza kielemu ambapo alisoma kozi fupi mbali mbali ikiwemo ya sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na Uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alihitimu stashahada ya juu ya Utawala mnamo mwaka 1986.
Kati ya mwaka 1992 mpaka 1994 Samia Suluhu Hassan alisoma stashahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Manchester kilichopo nchini Uingereza.
Kiu ya Mama Samia Suluhu Hassan kujiendeleza kielemu haijawahi kufikia ukomo kwani mwaka 2015 alihitimu shahada ya uzamili katika maendeleo ya uchumi ya jamii katika program ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo kikuu cha Southern New Hampshire cha nchini Uingereza.
Samia Suluhu Hassan aliolewa miaka miwili tu baada ya kuhitimu elimu yake ya sekondari kule visiwani Zanzibar mnamo mwaka wa 1978, ambapo alifunga pingu ya maisha Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo Wawili hao wamejaliwa watoto wanne ambapo Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir aliyezaliwa mwaka 1982 ndiye anayefata nyayo za mama yake kwani , ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar
Samia Suluhu Hassan mbali na kuhudumu Serikalini tangu amalize masomo yake ya sekondari akiwa na miaka 16 alipata kufanya kazi na mshirika ya kimataifa ambapo kati ya Mwaka 1992 mpaka mwaka 1994 alifanya kazi na shirika la umoja wa mataifa la mpango wa Chakula ambapo alihudumu kwa nafasi ya Afisa Miradi,Mbali na kufanya kazi Serikalini na katika shirika la umoja wa mataifa,Simia alipata kufanya kazi na taasisi zisizo za kiserikali kwa miaka karibu kumi akijikita zaidi katika harakati za usawa wa kijinsia
Bi. Samia alijiunga rasmi na siasa mwaka wa 2000
Alijiunga rasmi na siasa mwaka wa 2000 wakati alipochakuliwa kwenye baraza la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.,kuingia kwake kwenye siasa kuliifanya nyota yake kuanza kuchomoza katika medani za kisiasa na uongozi ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya akateuliwa kuwa waziri wa Afya, Jinsia na Watoto,uteuzi uliofanywa na Rais wa kipindi hicho Aman Karume
Mwaka 2005 alichaguliwa tena kuwa mjumbe maalum na kuteuliwa upya kama waziri, wakati huu akipewa wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji katika serikali ya visiwani..Mwaka wa 2010 alitia nia ya kuwania uwakilishi ambapo alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi huko Zanzibar.
Nyota ya Samia ilivuka mipaka kwani mwaka muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 alichomoza kwenye baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihudumu chini ya Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal.
Machi mwaka 2014 Tanzania iliingia kwenye vuguvugu la kubadili Katiba yake ambapo huko nyota ya Samia ilichomoza tena ,baada ya kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma. Bi Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour ambaye alipata kura 126 sawa na 24%. Itakumbukwa Samia Suluhu Hassan wakati wa Bunge la Katiba kwani ndipo alipoanzwa kutabiriwa kushika nafasi ya juu zaidi ya kiutawala ambapo mmoja wa wajumbe aliwaasa wajumbe wamfikirie Mama Samia kwa nafasi ya juu zaidi kwenye uchaguzi uliokuwa unafuata wa mwaka 2015.
Nyota ya Samia Suluhu haikuwahui kuzimika wala kufifia kwani Julai mwaka 2015, Dkt John Magufuli mara baada ya mpambano mkali ndani ya CCM uliompa ushindi wa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchauzi Mkuu wa mwaka huo,mbele ya wajumbe wa mkutani Mkuu alimpendekeza Mama Samia kuwa mgombea mwenza wake na hatimaye baada ya uchaguzi Samia Suluhu Hassan aliweka historia nyingine ya kupanda katika siasa za Tanzania kwa kwa chama chake kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliomuweka Samia katika historia nyingine ya kua msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maana ya Makamu wa Rais.
Mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati akiomba ridhaa ndani ya Chama chake ili apeperushe tena bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huo, kwa mara nyingine alimpendekeza Samia Suluhu kuwa mgombea mwenza wake ambapo ushindi wa chama chake uliilinda historia ya Mama Samia.
Kwa sasa,ndiye Rais wa Sita baada ya Julius Nyerere,Ally Hassan Mwinyi,Benjamini Mkapa,Jakaya Kikwete na John Magufuli,ambapo anashikashika nafasi ya juu kabisa ya kiutawala na kiuongoza baada ya kukidhi matakwa ya Katiba ya Tanzania.
Recent Comments