KISWAHILI LUGHA YA AFRIKA.
Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Saturday-24/04/2021.
Boma La Ngombe, Kilimanjaro, Tanzania
Moja ya lugha kubwa Afrika ni kiswahili, kiswahili ni lugha kubwa Afrika kwasababu ndio moja ya lugha chache ambazo asili yake ni Afrika, zaidi ya lugha 2000 zilizopo Afrika kiswahili ni lugha ya kwanza kwa ukubwa wa wazungumzaji ukiacha kiarabu.
Lakini…………….
Kiswahili ndio lugha ya kwanza yenye ASILI ya Afrika kuwa na wazungumzaji wengi, inawazungumzaji zaidi ya watu Million 250.
Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye mchanganyiko na misamiati mingine ya Kiarabu (30%), Kiingereza (10%) na lugha zingine kama Kijerumani, Kiuajemi, Kireno na kihindi, hili la lugha kuwa na mchanganyiko na lugha zingine (Utohaji) ni suala la kawaida Katika ukuaji wa lugha yoyoye ile duniani.
Kiswahili ni lugha inayozungumzwa hasa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki, na sehemu ya Afrika ya Kati.
Kimsingi lugha ya Kiswahili ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo, lugha ya Kiswahili ilianza kuandikwa kwa herufi ya Kiarabu pekee kwa karne nyingi, ukumbusho wa hilo upo kwenye Matini ya Sanamu ya Askari, Dar es Salaam.
Sarufi ya kwanza pamoja na kamusi ya mwanzoni ya kiswahili iliandikwa mwaka 1848 na Dokta Ludwig Krapf huko Rabai Mpya (Mombasa ya Sasa).
Kiswahili kilikuwa na lahaja nyingi kutokana na lugha mbalimbali za Kibantu zilizochangia katika eneo husika, tangu karne ya 19 lugha ilianza kuenea eneo la Afrika mashariti kwa njia ya biashara.
Wakati wa ukoloni wa Uingereza walianza jukumu la kuilasimisha lugha ya kiswahili kwa kuisanifisha.
Mwaka 1930 waingereza waliunda kamati yenye shabaha ya kuunganisha lahaja mbalimbali pwani za Afrika mashariki na kuunda Kiswahili cha pamoja (Inter-territorial Language (Swahili) committee for the East African Dependencies), Mwenyekiti alikuwa Frederick Johnson, makatibu R. K. Watts, P. Mzaba na Seyyid Majid Khalid Barghash.
Kamati hiyo iliamua kutumia lahaja ya Kiunguja kuwa msingi wa Kiswahili cha pamoja ambacho baadaye kialianza kufundishwa shuleni âstandard swahili ambayo leo ndiyo Kiswahili Sanifuâ kadhalika kikaanza kuandikwa vitabuni na magazetini.
Miaka ya ukoloni pia ilisababisha kupokelewa kwa maneno mapya katika Kiswahili, Kijerumani kiliacha maneno machache kama “shule” (Kijerumani Schule) na “hela” (Heller) Kiajemi pia kilichangia maneno mbalimbali, kama vile “bibi” na “cherehani”, Kireno kikaacha maneno kama “Meza”, “Karata” “Embe” na Kihindi kikaacha maneno kama “Pilau” na kadhalika, Kufika kwa Wareno kuanzia mwaka wa 1500 walileta maneno kadhaa ya Kireno katika Kiswahili kama vile “bendera” na “gereza”.
Kuwepo kwa wafanyabiashara Wahindi katika miji mikubwa ya pwani pia kuliingiza maneno ya asili ya Kihindi katika lugha kama vile “lakhi”, “gunia” chapati nk. Athira ya lugha za Kihindi iliongezeka kiasi baada ya Waingereza kutumia Wahindi wengi kujenga reli ya Uganda na wakati huo ndo kuliibuka neno âharambeâ lililotumika wakiinua reli.
Kuna wengine hudhania Kiswahili ni lugha changa na kusema âtukuze kiswahiliââ bila kujuwa lugha hii ilikuwepo hata kabla ya nabii Issa (BC), Historia pia yaonyesha kuwa kiswahili kiliandikwa kwa herufi za Kiarabu kwa muda mrefu tangu karne ya 13 BK, Hali ya hewa hasa pwani haisaidii kutunza karatasi na kurasa nyingi zenye maandishi ya kale zimeharibika kutokana na unyevu hewani maana tungo nyingi za watunzi wa kale zilipotea akiwemo Muyaka Bin Haji(1776 â 1840) , Alii Bin Athuman (Ali Koti 1776 1834) Zahidi Mngumi(1758-1828) n.k japo nyingine zilipotelea mikononi mwa baadhi watu waliokuwa wakihifadhi enzi hizo.
Lakini maandiko ya kale yanayopatikana kutoka karne ya 17 huonyesha ya kwamba tenzi na mashairi vinafuata muundo uliotangulia maandiko yenyewe kwa karne kadhaa, Sehemu kubwa ya maandiko ya kale ni tendi zenye aya maelfu, Utendi mrefu zaidi unahusu kifo cha Mtume Muhamad ukiwa na aya 45,000.
Asilimia 70% ya wazungumzaji wa lugha ya kiswahili ipo Afrika Mashariki, karibu watu million 150 huzungumza kiswahili, hasa kwenye nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mashariki ya Kongo DRC, kaskazini mwaka Msumbiji, visiwa vya Comoro, kusini mwa Somalia, kusini mwa Sudan kusini, kusini Mashariki mwa Ethiopia na Mashariki mwaka Zambia.
Kwa Tanzania, lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa, ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani, pia ndio lugha inayo tumika kote nchini.
Serikali inatakiwa kukiendeleza Kiswahili kwa sababu ni lugha ya taifa, Sera ya elimu ya mwaka 2015 imechagua Kiswahili katika miaka 10 ijayo kiwe lugha ya kufundishia katika ngazi zote, ikiwemo ile ya chuo kikuu.
Kwa Kenya, lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa tena lugha rasmi, sawa na Kiingereza, baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa tarehe 4 Agosti 2010, ilitamka kuwa Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo lenye kabila moja, ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni, ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa.
Sehemu za ibada zinatumia Kiswahili, kuna gazeti moja tu la Kiswahili nchini Kenya, Hata hivyo, lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au za kikabila.
Kwa nchi ya Uganda, kiswahili kimetangazwa kuwa lugha ya taifa tangu 2005, iliwahi kuwa lugha ya taifa wakati wa utawala wa Idi Amin, wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo.
Ni lugha ya polisi na jeshi pia nchini Uganda, Mwaka 2005 bunge lilipiga kura kukifanya kiswahili kuwa lugha rasmi ya pili kwa kuwa kinazungumzwa zaidi (nje ya Buganda).
Kwa nchi y Rwanda, Tarehe 8 Februari 2017 bunge la taifa hilo ilikifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne baada ya Kinyarwanda, Kifaransa na Kiingereza.
Kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kiswahili ni kati ya lugha tank (5) rasmi za kitaifa (pamoja na Kilingala, Kiluba, Kikasai na Kikongo), pia nchini Kongo kiswahili ni lugha ya jeshi.
Kiswahili kilifika mashariki ya Kongo na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani ya Tanganyika tangu karne ya 16, lakini pia kiswahili nchi Kongo huzungumzwa zaidi Katika maeneobya mashariki mwaka Kongo na kusini mwaka Kongo Katika jimbo la Katanga.
 Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu.
 Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
®Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
© Copyrights of this article reserved
®written by Comred Mbwana Allyamtu
â¢Napatika Kwa mawasliano
â¢Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Email-Â mbwanaallyamtu990@gmail.com
© Copyright 2021, All Rights Reserved.
Recent Comments