Kigoma. Secretarieti ya kuzuia na kupambana na usafirishaji haramu wa Binadamu kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa [I O M], limeanza utekelezaji wa Mkakati wa kukabiliana na Biashara hiyo ambayo imeanza kukua kwa kasi kwa Tanzania kwa kuifanya kuwa njia kuu ya kupitishia Watua kwenda Ulaya na Nchi za kusini mwa Afrika
 Mkuu wa Kitengo cha utafiti na Takwimu wa Secretarieti hiyo Alexanda Lupilya wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa kupambana na biasahara ya usafirishaji haramu wa Binadamu uliofanyika Jana Manispaa ya Kigoma, amesema Mkakati huo ni Pamoja na kutoa Elimu kwa Maafisa wa Secta zote zinazohusiana na usafirishaji wa Binadamu Pamoja na kutumia sheriazilizopo na za Kimataifa kuzuia Biasahara haramu ya Magendo ya Binadamu ambayo imekuwa ikiathiri uchumi na Maisha ya Watu
Halima Sonda Afisa kutoka shirika la uhamiaji la Kimataifa Tanzania, amesema kwa hapa Tanzania shirika hilo limekuwa limekuwa likishirikiana na Taasisi mbalimbali  kueendesha Mijadala mbalimbali ili kuhakikisha Jamiii inakuwa na uelewa ili iweze kujiepusha na masuala ya usafishaji haramu bali sheria zitumike
ââUshirikiano wa Wadau katika kupiga Vita Biashara hii unahitajika sana vikiwemo vyombo vya Dora ili kukomesha hali hii ikiwa ni Pamoja na utoaji elimu kwa jamii kuanzia ngazi zote katika maeneo ya Mijini na Vijijini ili Watu wengi waweze kuepukana na vishawishi mbalimbaliââalisema Sonda
Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Ilvin Mugetta amewataka Wadau wa Udhibiti wa usafirishaji haramu wa Binadamu katika Mkoa wa Kigoma, kuhakikisha sheria na Mikataba ya Kimataifa zinafuatwa wakati wa utekeleza wa Mkakatihuokatika Mkoa wa Kigoma ambao umekuwa lango la Wageni kutoka Nchi Jirani na kueleza kuwa Watanzania wanatakiwa kufuata taratibu za uhamiaji kwa hakuna anayezuiliwa kufanya kazi nje ya nchi
Hata hivyo baadhi ya Wananchi Jovin Bonajose na Dickson Herman  walikuwa na maoni kuwa jambo kubwa linalopelekea kuwepo na usafirishaji haramu wa Binadamu tena kwasi ni kutokana hali ya umasikini unaozikumba jamii za Afrika hasa kwa wanawake Wasichana na Watoto ambao mara nyingi ushawishika kwa haraka yakiwemo makundi yote ya Vijana
Mara nyingi Wafanyabiashara husika uja kwa lugha za kuonyesha utajiri kwa wahanga iwapo kama watakubali kusafirishwa kwakuahidiwa kazi nzuri na mara wanapo kubali na kufikishwa kule walikoelezwa kwenda ukuta hali ni tofauti wengi kufanyishwa kazi ngumu, kama ngono, na nyinginezo huku wakinyimwa mishahara yao na suala hili mashirika na serikali yasiangalie nchi za nje pekee bali hata ndani ya nchi yapo matendo ya biashara hizo yanafanyikaââalisema Herman
Mwisho
Recent Comments