Mgombea Ubunge Jimbo la Buhingwe Mkoani Kigoma kupitia chama cha Mapinduzi Eliadoli Felix amewataka wakazi wa jimbo hilo kumwamiani kuwa atawaletea maendeleo maana amejipanga Vizuri kuliendeleza Jimbo hilo katika Nyanja mbalimbali
Akiongea kwenye Kampeni za uchaguzi Mdogo zinazoendelea Jimboni humo akiwa kwenye Kata ya Kinazi Felix amesema Pamoja na ubunifu alionao  anataraji kutumia mwongozo wa chama hicho ambao ni Ilani katika kuboresha Maisha ya Wana Buhigwe
âNitajitahidi kabla sijaenda Bungeni nita sikilikza kero za Wananchi na maoni yao, tutakaa pamoja na kujadili na kisha nitapeleka maoni hayo na kero zitakazokuwa zimetolewa ili ziweze kupatiwa ufumbuzi, maana natambua licha ya maelezo ya Ilani zipo changamoto nyingi tu ambazo zinatakiwa kutazamwa kwa jicho la Pekee, hivyo iwapo nitapata lidhaa ya kuogoza Jimbo hili nitajitahidi kuwa Pamoja nanyi Wananchi
Nao baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kinazi Ruth Kisamuhala na Deus Kilaha wamesema zipo changamoto za upatikanaji wa huduma za Afya hasa Madawa katika Vituo vya kutolea huduma za afya, Maji nyakati za Kiangazi yanapatikana kwa shida ambapo wamesema wanahitaji Mbunge atakayeweza kutazama changamoto hizo Sugu
ââMatatizo hasa upatikanaji wa Madawa kwenye Vituo vyetu, umekuwa ni wimbo usiyoisha Pamoja na maji ni shida maeneo mengi huku kwetu tumekuwa tukihangaika sana na tumekuwa tukipata adha kubwa Wasichana na wake zetu wamekuwa wakitumia muda mrefu kutafua majiââ alisema Kilaha
Uchaguzi huo mdogo unafanyika kutokana na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Philipo Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupelekea kukosa sifa za kuwa Mbunge wa jimbo hilo kisha kusha kutangazwa uchaguzi mdogo, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika May 16 2021
Recent Comments