Kampeni za kuwania Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Muhambwe Kibondo Mkoani Kigoma, zimeendelea kushika Kasi kwa kuwanadi wagombea nafasi hiyo kupitia katika Vyama vya Ccm na Act Wazalendo
Kwa chama cha Act Wazalendo Mgombea wake Julias Masabo amefanya Mikutano ya katika Kata za Murungu na Biturana ambapo amesema kutokakana changamoto za ukosefu wa Masoko ya Mazao mbalimbali yanayolimwa wilayani humo iwapo atapata lidhaa ya kuongoza Jimbu hilo atahakikisha anaboresha Vituo vya biashara maeneo ya Mpakani ili wananchi waweze kunufaika na kilimo
Baadhi ya Mazao hayo ameyataja kuwa ni Mhogo, Maharage na Mahindi ambayo yamekuwa yakilimwa kwa kiwango kikubwa lakini masoko yake ni kidogo ikilinganishwa na garama ambazo wamekuwa wakitumia wakulima wakati wa Kilimo
Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi ambacho mwakilishi wake Frolence Samisi alieendesha Kampeni zake katika Kata ya Mabamba amesema iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge wajimbo hilo la Muhambwe atahakikisha anaishawishi serikali inapelekea Umeme kwa wakatikati katika Vijiji vya jimbo hilo ili kusadia wananchi ambao wamekuwa wakihitaji Nashati hiyo
Frolence amesema zipo changamoto za afya ambazo mara nyingi wanbanchi wamekuwa wakipata adha kubwa katika kupata huduma za afya hasa kwa wananwake na Watoto na kwa kuwa suala la  utoaji  huduma bora za afya lomo katika Ilani ya Chama chake, atashirikiana na serikali kuondoa changamoto hizo zinazowakabili wananchi
Feb 12 mwaka huu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Atashasta Nditiye alifariki Dunia kwa ajali ya Gari huko Mkoani Dodoma na kupelekea Jimbo hilo kuwa wazi na baadae kutangazwa na Tume ya uchaguzi kuwa linatakiwa kujazwa na sasa vyama vilivyopata Fulsa ya kupeperusha Bendera, kwa sasa vipo katika ushindani
Recent Comments