Katika  mwaka wa masomo wa 2021/22 Mkoa wa Kigoma unakabiliwa na upungufu wa madarasa 1010 katika shule za sekondari kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza mwakani huku idadi ya madarasa iliyopo kwa sasa ni 404.
Hayo yameelezwa na katibu tawala wa Mkoa huo Rashidi Kassim Mchata wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi kutoka kwa wadau wa maendeleo nchini ili kukabiliana na upungufu huo.
Amesema makadilio ya kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi watakao ingia kidato cha kwanza hapo mwakani ni Zaidi ya asilimia 85 na hivyo kufanya idadi ya miundombinu ya madarasa iliyopo kwa sasa kushindwa kukidhi mahitaji ya wanafunzi hao.
Serikali kupitia halmashauri zote nane mkoani Hapa pamoja na wananchi wameanza ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika baadhi ya shule ili kuhakikisha wanafunzi wanaanza masomo kwa wakati kama inavyoelezwa na mkurugenzi wa halmashauri ya kasulu Joseph Kashushura.
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya kibiashara ya NBC Theobal seobal baada ya kukabidhi mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani Kigoma amesema wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu hasa ya elimu.huku Baadhi ya wananchi Samweli Masunzu na James Ntoteye wakitoa pongezi kwa Benk hiyo kutokana na msaada huo kwani utachangia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa na kupunguza adha kwa upande wao
”Kama inavyofahamika Shule za Msingi na sekondari za Kata ni zinamilikiwa na jamii katika maeneo husika na wananchi tumekuwa tukichangia katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa hivyo msaada huu utaongeza nguvu kubwa katika kuboresha shule zetu” amesema James
Recent Comments