Na,SALVATORY NTANDU-SHINYANGA
Mwanaume mmoja Mkazi wa mtaa wa Ndembezi manispaa ya Shinyanga anayetuhumiwa kuwa ni jambazi sugu, Idd Masasi (43) ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika tukio la  majibizano ya risasi wakati akijaribu kuwatoroka polisi baada ya kukataa kujisalimisha kwa vyombo vya usalama.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi (ACP) Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo mei 31 mwaka huu na kusema kuwa Idd anatuhumiwa kufanya matukio ya uhalifu ya unyangâanyi wa kutumia silaha katika mikoa ya Shinyanga na Dar es salaam.
âJeshi hilo lilipata taarifa za siri za uwepo wa jambazi (Idd Masasi) ambaye alikuwa anatafutwa na jeshi la polisi  makosa ya unyangâanyi wa kutumia silaha hasa matukio yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo ya kigamboni na Dar es salaam na kisha kukimbilia mkoani Shinyanga,âalisema Magiligimba.
Alisema kuwa taarifa za kutafutwa kwake zilifunguliwa katika vituo vya Polisi kigamboni kwa kumbumbu za vitabu namba  KGD/IR/1050/2021, KGD/IR/411/2021 ambazo zilifunguliwa kwa lengo la kuendelea kumtafuta ili aweze kufikishwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama baada kutoroka baada ya kutekeleza uhalifu huo.
âBaada ya kupata taarifa askari wetu wakishirikiana na kikosi kazi cha askari kutoka jijini Dar es Salaam liliweka mtego maeneo ya soko la Nguzo Nane na ambapo majira ya saa tano alipofika katika eneo hilo na aligundua anafuatiliwa  alianza kukimbia ndipo askari walipompa ilani ya kusimama kwa kufyatua risasi hewani lakini alikaidi,âalisema Magiligimba
Kamanda Magiligimba amesema kuwa askari waliamua kumfyatulia risasi mbili bila kuleta madhara kwa watu wengine waliokuwepo eneo hilo, risasi hizo zilimjeruhi mguu wa kushoto na sehemu ya mgongoni na kisha  kumkamata na kupelekwa hospitali ya mkoa kwajili ya matibabu na alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu.
Nitoe onyo kwa waharifu wote kuwa mkoa wetu siyo sehemu rafiki ya kutenda uharifu au kukimbilia waharifu kujificha baada ya kufanya uharifu mikoa mingine kwani jeshi la polisi limejipanga vizuri kukabiliana nao, aidha mharifu yeyote atakayethubutu kufanya uharifu atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, waharifu wote wafahamu kwamba sehemu ambayo wapo na sisi jeshi la polisi tupo,â alisema Magiligimba
Kamanda Magiligimba amefafanua kuwa kumbukumbu za polisi zinaonesha kuwa Idd alishawahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyangâanyi wa kutumia silaha mwaka 2011 na kutumikia adhabu hiyo katika gereza la Butimba, Mwanza na baadae alitoka kwa rufaa.
Recent Comments