Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza mikakati ya kuwekeza majengo ya kibiashara katika maeneo ya mipakani.
Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 6, 2021 na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt Maulid Banyani wakati wa uzinduzi wa Nyumba za Makazi katika eneo la Buhare wilayani Musoma mkoani Mara uliofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula.
âMheshimiwa Naibu Waziri, kama ulivyoelekeza kwamba, Shirika liwekeze majengo ya biashara maeneo ya pembezoni mwa nchi yetu, tulishaanza kufanya hivyo eneo la Mutukula, Kagera na sasa tunaangalia uwezekano wa kuwekeza kwenye mpaka wa Kenya na Tanzaniaâ alisema Dkt Banyani.
Kwa mujibu wa Dkt Banyani, Shirika lake kwa sasa linafanya upembuzi yakinifu eneo la Sirari mpaka wa Tanzania na Kenya na uamuzi huo unatokana na timu iliyofanya ziara katika eneo hilo kukuta upande wa kenya umechangamka kibiashara ukilinganisha na ule upande wa Tanzania.
Alisema, Shirika la Nyumba la Taifa likiwezeshwa ikiwemo kupatiwa ardhi kwa ajili ya uwekezaji majengo litafanya mabadiliko makubwa na kutolea mfano wa jengo la TRA lilipo mpaka wa Tanzania na Kenya haliko vizuri ukilinganisha na lile la Kenya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika uzinduzi huo alisema, mbali na mikakati ya shirika la Nyumba kuwekeza majengo ya kibiashara, halmashauri zilizoko maeneo ya pembezo zinapaswa kuitumia NHC kwa kulipatia ardhi ya kufanya uwekezaji.
âPamoja na mikakati ya uwekezaji maeneo ya pembezoni iko haja ya kulitumia shirika la nyumba la taifa kwa kuliwekea miundombinu mizuri ya kibiashara ili liweze kuwekeza maeneo ya mipakani ampapo Tanzania inaonekana iko nyuma ukilinganisha na nchi jiraniâ alisema Dkt Mabula.
Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi alielekeza kujengwa shule ya msingi ya serikali katika eneo la Buhare zilipozinduliwa nyumba 50 baada ya kuombwa kufuatia eneo hilo kutokuwa na shule. Eneo hilo la Buhare lina ukubwa ekari 135 na zilizotumika ni ekari kumi pekee.
Vile vile, Dkt Mabula alitaka maeneo ambayo Shirika la Nyumba linafanya miradi yake, halmashauri husika zihakikishe linawezesha upatikanaji miundombinu kama vile umeme, maji na barabara kwa lengo la kupunguza gharama za upangishaji au uuzaji wa nyumba za shirika la Nyumba la Taifa.
Recent Comments