Chama cha watu wenye ulemvu Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera kimegawa Kadi za BIMAÂ ya Afya kwa watoto watatu wenye matatizo ya Vichwa vikubwa ikiwa ni kuwapunguzia wazazi na walezi wao gharama za matibabu
Akitoa taarifa ya upatikanaji wa kadi hizo zinazotamburika kwajina la TOTO KADI,Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ulemavu Bw.Deogratius Andrew Francis amesema BIMA hizo zimetokana na ufadhili wa Shirika la Foundation for Disabilities Hope lenye makao makuu Dodoma
Amesema kupatika na kwa Bima za watoto hao kutapunguza changamoto walizokuwa wanakutana nazo kwakuwa matibabu ya watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa yanagharimu kiasi kikubwa cha Pesa
Akizungumzia upatikanaji wa BIMA hizo,mratibu wa Mfuko wa BIMA wilaya ya Ngara Bw.Felix Francis amekitaka chama cha walemavu kushawishi Shirika lililowafadhili kuanzisha Ofisi Wilayani Ngara ili kurahisisha huduma kwa walemavu wengine.
Recent Comments