Ninapenda kutumia fursa hii kuwatakia Mtihani mwema Wanafunzi wa darasa la saba wanaoanza mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi kesho tarehe 08/09 /2021Â na kumaliza keshokutwa tarehe 09/09/2021.
Watoto wetu ninawapenda sana hivyo ninawatakia kila la kheri, neema na baraka tele na ninawaombea Mwenyezi Mungu awasaidie waianze na kuimaliza salama.
Imani yangu watafanya vizuri sana kwa kuwa wameandaliwa vya kutosha na Walimu wenye uzoefu na umahili wa hali ya juu sana.
Ninatoa wito kwa Walimu, Wanafunzi na Wasimamizi wa mitihani hiyo kutojihusisha kwa namna yoyote ile na vitendo vya udanganyifu ama wizi wa mitihani hiyo kwani ni kosa kisheria na kwa atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Sambamba na hilo pamoja na kwamba Serikali inatekeleza sera ya elimu bila malipo, ninatumia nafasi hii kuwakumbusha Wazazi kuwa kufanyanyika kwa mitihani hiyo ni kengele inayowakumbusha kuwa na utayari wa kufanya maandalizi mapema ya mahitaji ya Wanafunzi kwa wale watakaofaulu kujiunga na Kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo unaonza Januari 2022.
Recent Comments