Leo nikujuze tu vyakula vya asili ni muhimu sana kwetu japo watu wengi hushindwa kuvitumia kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, utandawazi, biashara na mengineyo.
Kwa sasa watu wengi hasa wa mijini hawapendelei kabisa kutumia vyakula asilia na kupendelea vya mabara ambavyo nibhatari sana katika miili yetu kwasababu ya kemikali zinazotumika, hivyo hupelekea kushuka kwa kinga ya mwili.
Watu huwa tunapendela sana matumizi ys bidhaa toka nje ya Tanzania kama vile tambi na vinginevyo bila kupima athari na ibora wa bidhaa hizo na mwishowe kuhatarisha afya zetu kwa kuwa bidhaa nyingi za nje zina kemikali nyingi hatare kwa afya mfano mtu anaona anunue Tufani (apple) la South Africa siyo la Tanga ambapo hilo la South Africa lina Kemikali ili lituzike.
Madaktari mbalimbali na watalamu wengi wa lishe wanasihi watu kwamba, Baadhi vyakula vinavyoletwa kutoka nje ni hatari kwa afya zetukwa kuwa vinakuwa havina ubora thabiti pia hutumia Kemikali nyingi ili kutunza ambazo huathiri miili yetu.
Moja ya kazi ya vyakula vya asili ni kuleta nguvu na kulinda mwilini ndio maana mababu zetu walikuwa na nguvu na afya imara kutokana na kula vyakula asili bila mchanganyiko na bandia.
Kwa sasa vyakula asilia vimekuwa na bei hii ni kutokana na kuongezeka kwa vyakula bandia masokoni na kufanya asilia kuwa adimu sana
Ili kuboresha afya zetu na kuongeza umri wa kuishi tunahitaji lishe bora ambapo lishe bora ni matokeo ya vyakula bora vinavyozalishwa na kuhifadhiwa katika mazingira safi na salama. Hivyo basi ni vyema kuchunguza ubora na usalama wa chakula kabla ya kukitumia vilevile mamlaka husika ziongezee umakini na kutilia mkazo ukaguzi wa bidhaa hizoo ili kuhakikisha usalama wa wananchi.
Vilevile ni vyema kutumia vyakula vya asili vinavyolimwa bila ya kemikali kujiepusha na uwezekano wa kupatwa na magonjwa mbalimbali pia kuimarisha afya ya mlaji.
Ni vyema kula zidi vyakula asilia ili kulinda afya zetu kwa kuwa vyakula vya asili ni kichocheo bora cha kinga za miili yetu.
@Ventas Malack
Recent Comments