Rais Samia Suluhu Hassan amewaambia panya road waache mara moja matukio ambayo wamekuwa wakiyafanya mana yanahatarisha sana maisha na usalama wa raia na mali zao katika jamii.
Raisi Samia amesema hilo alipokuwa akihutubia maelfu ya wafanyakazi jana katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika jijini Dodoma siku ya jana ambapo alizungumzia suala hilo baada ya kusikika kwa matukio kadhaa wiki iliyopita yaliyohusisha hao panya road.
Kiuhalisia matukio yatokanaayo na panya road huwa ni hatari maana wao huvamia na kupora mali na pia kushambulia watu ambapo Rais Samia amewaonya waache tabia hiyo mapema.
Suala la ulizi ni jukumu la wote siyo serikali tu au jeshi la polisi pekee ila jukumu hilo linatakiwa kuwa la jamii nzima kwa ujumla hivyo jamii inalazimika kuungana na kushirikiana ili kulimaliza suala hilo la panya road.
Recent Comments