Nazir Mustafa Karamagi alizaliwa tarehe 13.12.1953 Kijiji cha Nyakabanga kilichopo kata ya Butelankuzi, Wilaya ya Bukoba Vijijini; Mkoa wa Kagera.
*Nazir Karamagi ni msomi mzuri.*
Alipata Elimu ya Msingi Shule ya Rubale, Elimu ya Sekondari Shule ya Nyakato (Kagara) kidato cha 1 mpaka cha 4 na kidato cha 5 mpaka cha 6 Shule ya Sekondari Kibaha.
Alipata Elimu ya juu ngazi ya Masters Degree tatu:
Ya kwanza toka Chuo Kikuu cha Madini cha St Petersburgh (Urusi) na kutunukiwa Shahada ya uzamili (Masters Degree) ya Uhandisi mitambo ya Umeme, ya pili toka Chuo Kikuu cha Edimburgh (Uingereza) na kutunukiwa Shahada ya uzamili (Masters Degree) ya Utawala na kusimamia Biashara na ya tatu toka Chuo Kikuu cha Strathclyde (Uingereza) na kutunukiwa Shahada ya uzamili (Masters Degree) ya Uchumi na Fedha.
Ukiangalia mazingira ya sasa ya dunia na hasa Tanzania na hususan Kagera, tunahitaji viongozi wenye upeo mpana wa kuweza kutuelekeza katika njia sahihi za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Hili halihitaji elimu tu bali hata viongozi wenye uzoefu wa kivitendo na mahusiano kwenye serikali na sekta mbali mbali za umma na sekta binafsi za kitaifa na kimataifa.
*UZOEFU*
Nazir Karamagi ana Uzoefu mkubwa wa Sekta ya Umma:
Kwa miaka 7 toka mwaka 2003 â 2010 amekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini kwa tiketi ya CCM.
Katika kipindi chake cha ubunge, aliteuliwa kuwa *Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko* na baadaye kuhamishwa wizara na kuwa *Waziri wa Nishati na Madini.*
Katika Sekta Binafsi, Nazir Karamagi ni mjasiliamali na mwekezaji aliye bobea. Aliwahi kuwa *Mkurugenzi katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),* na mpaka sasa ni mjumbe wa Bodi mbali mbali za kitaifa na kimataifa.
Nazir Karamagi amewekeza katika miradi mbali mbali ikiwemo katika makampuni yaliyomo katika Soko la Mitaji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange), katika kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services Ltd (TICTS) kampuni inayoendesha kitengo cha makontena katika Bandari Kuu ya Dar es Salaam, kampuni ya Tanzania Microfinance inayo shughulika na kutoa mikopo kwa wafanyakazi na wajasiliamali wadogo wadogo n.k.
Ndani ya Mkoa wetu wa Kagera, Nazir Karamagi amewekeza katika kiwanda cha Maji na Juice eneo la Kashai katika Manispaa ya Bukoba.
Nazir Karamagi vile vile ni Mkulima na mhamasishaji wa kilimo cha zao la Parachichi katika mkoa wa Kagera.
Hizi ni kati ya juhudi zake za kufanya Parachichi liwe moja wapo ya zao la kibiashara la kimkakati Mkoani Kagera katika mbinu za kupambana na umaskini unaosemekana kuukumba mkoa wetu.
Mh Karamagi anamiliki Shamba lenye kama eka 30 linapatikana katika Kijiji cha Itahwa, Kata Karabagaine Bukoba Vijijini.
Kupatikana kwa mabadiliko chanya Mkoa wa Kagera yanahitaji viongozi wenye maono na uwezo wa kuunganisha mambo yafuatayo kwa pamoja: Kuhamasisha umma kwa vitendo, kuzielewa vizuri Sera za Chama Cha Mapinduzi na zinavyo shughulikiwa na Serikali yake na mchango wa Sekta binafsi katika uchumi wan chi.
Kwa ngazi za Chama anao uzoefu ufuatao. Nazir Karamagi anatambulika kwa ushiriki na michango yake mingi ya hali na mali katika Chama chetu cha CCM na jumuiya zake.
Aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tawi la Umoja wa Vijana (Tanu Youth Legue) la Shule ya Sekondari ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, Mmojawapo wa wanachama watano nchini walio teuliwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi kuwa Makamissari katika Viwanda vya Kimkakati nchini. Uteuzi huu ulidumu hadi Tanzania ilipokumbatia mfumo wa vyama vingi.
Nazir Karamagi alikuwa *Mjumbe wa Halmashuri Kuu ya Taifa (MNEC)* toka Mkoa wa Kagera kwa miaka 15 (2002 â 2017).
Michango ya Karamagi katika chama ni mingi kuitaja lakini ambayo ni vigumu kusahaulika ni *kama ile ya kuwezesha kukomboa Jengo la CCM la Mkoa lililokuwa limeshikiliwa na mkandarasi kwa madai ya shilingi milioni 86,* kuchangia gharama zilizokuwa zinahitajika ili kupatikana kwa gari la Mkoa na Wilaya ya Bukoba Vijijini, kuanzisha mfuko wa mkoa wa upatikanaji wa kadi za CCM n.k
Kwa kumaliza tukumbuke kuwa Mkoa wa Kagera kwa sasa unakabiliwa na changamoto ya kuwa mkoa wa kwanza kwa umaskini katika mikoa yote 26 ya Tanzania. Hii ni aibu sana na hatuwezi kukubali kuendelea kuibeba kama wana kagera.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM alipotembelea Mkoa wetu, alituachia changamoto ya kumweleza tumejipangaje na tunahitaji nini ili serikali ikaingilie kati kutusaidia.
Jambo hili ni kubwa kwa masilahi ya Wana Kagera wote. Hoja iliyopo ni viongozi gani wa CCM wana uelewa na uwezo wa kuongoza na kusimamia zoezi hili ikiwemo kuvutia uwekezaji?.
Kwa sasa tunahitaji kiongozi kama Karamagi ambaye anakidhi vigezo vyote kwa sifa na uzoefu vya kutuletea mabadiliko ya kiuchumi katika Mkoa wetu wa Kagera.
Imeandaliwa na Frank Partson Mwana CCM na mchambuzi huru wa mambo ya kisiasa.
Sure Karamagi atawafaa sana.huyo mkaka alikuwa room mate wa Kaka yangu IFM (Evance Zera rip) yupo poa.
Mtu muhimu sana kwa kagera ya leo.
Naziri Karamagi