Na Kufuri Mwenye Kamera Nene, Wilani Ngara
Ni saa kumi na moja alfajiri nikiwa nafanya jogging, na nimemuona aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Ngara, Ndg Juventus Juvenary akiwa anaelekea shambani kwake na wasaidizi wake. Pia siku hizi kwenye vibanda vya kahawa hapa Wilani Ngara, Ndg Juventus Juvenary anaonekana ana furaha na kashasahau uchovu unaotokana na shughuli za kuandaa mazingira mazuri ya boss wake pale anaporudi wilayani kutoka Dodoma. Siku hizi, Ndg Juventus anaona kuwa na furaha kabisa – stress free na anatumia muda wake kwenye kilimo na shughuli nyingine zinazomuweka karibu na jamii yake.
Sasa swali linaloulizwa na wengi ni siri ya mafaniko ya Ndugu Juventus Juvenari kutokana na uhuru aliokuwa nao baada ya kuacha kazi ambayo pengine ilikua kama kifungo cha raha na kilichotumia muda wake mwingi. Ama hizi furaha tunazozishuhudia mtaani ni zao la pochi nene Mheshimiwa Mbunge aliyompatia kijakazi wake kama kiinua mgongo? Ama tulidhishwe na ule ubeti eti mheshimiwa anaupiga mwingi maana ameachisha kazi mtu aliyekua anamzidi umarufu ndani na nje ya Ngara?
Hizi ni duku duku za wana Ngara na pengine hatutopata majibu sahihi muda huu. Ila nakumbuka ni siku change tuu Video ilisambaa mitandaoni ikimuonesha Mbunge wa Ngara Bw. George Ndaisaba Ruhoro akitembea kwenye mashamba ya Parachichi. Aliyekua Katibue wa Mbunge, Ndg Juventus Juvenary alipokea ujumbo kutoka kwa bosi na kuja kwenye jamii kuutimiza kwa vitendo kama anavyoonekana kwenye hii video akiwa shambani kwake.
Swali lililopo kutoka kwa watalaam wa kimataifa ni kama kilimo ni mpenyo sahihi kwa vijana wengi waliopo Africa? Kama kilimo cha mkononi na mdomoni kweli kitafanikisha mategemeo ya waafirca wengi huku vitendea kazi na virutubisho vya mazao ni haba?
Uhaba wa watalaam wa kilimo kutoonekana mashambani, tozo kuwa nyingi hata kwenye virutubisho vinavyohitajika kuboresha shughuli za kilimo.
Mheshimiwa Katibu Mstaafu, Ndg Juventus Juvenary ameamua kuungana na wananchi hasa baadhi ya Vijana waliojikita kwenye Kilimo baada ya kusomeshwa namba kwa muda mrefu – ila huu ni mtazamo wangu binafsi. Pengine shughuli zake zitamuwezesha kumudu mahitaji yake yote.
Jitihada za Simamia.com hazikuzaa matunda zilipojaribu kumpata Bw. Juventus Juvenary ambaye katika mitandao ameonekana kujikita shambani na kusogeza jamii yake kwa ukaribu sana. Simu zote za huyu kinara kwenye journalism na kwenye kuunganisha jamii hazikupatikana. Pia mtandao wa ngara tv, ambapo Mstaafu Katibue Juvenary Juventus ndipo anatumia ujuzi wake mahili kung’alisha wale anaowasadia – kwa bahati mbaya haupatikani na simamia.com haikuweza kuwafikia wahusika katika kuchangia kwenye hii habari kabla haijapepereushwa.
Wahusika mnakaribishwa ofisini Kabanga kama mnachochote cha kuchangia.
Pia tutashukuru ukitumia lugha nzuri kutoa comments hapa chichi.
*Ni mwandishi mwenye kamera nene, Kufuri.
Ndugu mwandishi hujanitendea haki hata kidogo. Habari yako haijashiba. Ili uandike habari unatakiwa kuzingatia mambo mengi. Kwanini nisikupekeke mahakamani?
Simamia asante kwa kazi zenu ila hizi kazi za siasa ni tumbo mtupu. Pengine Juventus alikua analipwa vizuri na alikua na heshima yake kubwa tuu alipokua Kwizera. Hizi kazi za wilayani ni heshima ya mdomoni na ya kuvaa tai tuu. Hao wameshindwa hata kumpatia maji kwenye viroba na kuuyauza kama ice.
Pengine huyu mzee atanenepa na kunawili akiwa nje ya siasa. Leo nendeni na mkapige picha nyumbani kwake. Halafu rudini miaka mitano mchumue picha halafu zinganisheni. Mtakuta Luna hatua ya maendeleo. Hapo kalinganisha ujinga wa kunyenyekea nyekea mambo yanaoungana kwenye maandishi ila hayakubali kuunganishwa practically akaona ajikume. Hii nchi bila katiba mpya mambo hayatosogea. Tutaendelea kuzunguka msitu na bado tupo pale pale.
Pili Juventus hiyo nafasi haikumfaa. Juventus amekuwa anafanya kazi na makampuni makubwa, anakin kubwa kuliko mkuu wa wilaya, sembuse hugo mbunge anayezubaishwa na koti aliloazima kwa miaka mitano. Juventus alikua ana mu overshadow tuu.
Pili Juventus hapokeagi tharau kutoka kwa mtu yoyote. Ndio anaweza kuwa wanaonekana ni mkimya ila yeye sio zumbu kuku kama hao wengine wakisikia neno Mbunge wanashituka mama vile wameguswa kwenye kovu.
Pia ieleweke makatibu kadhaa toka wilaya za pembeni nao walijihuzuru ama hawapo tena na wabunge. Kama mbunge hata katibu wako anakudharau na kujihuzuru, wewe kweli inafaa? Unashindwa kuongoza baraza lako kesho ndio utasogeza matege yako eti upewe awamu nyingine huku waliokuzunguka wamekuona ni hopeless? Ni muda wa kujitafakari na kuacha kujidanganya, wewe jimbo limeshakushinda.
Hongera sana Juve, rudi Ngaratv ukaguse guse ule waya ili ngaratv ifufuke. Ukiona vipi jirudie Kwizera ama kufa na shughuli zako za kibiashara. Unefanya uamuzi mzuri sana. Simamia ninawakubari, endeleeni kuwakilisha Wilaya na mkoa wetu. Nyosheni palipopinda, Maine kama wale wanaoishi kuabudu tuu. Tuwekeni kwenye ramani ya ulimwengu. Hakika Ngara tumebarikiwa kuwa nanyi na muendelee kubalrikiwa.
Good story ebu katembelee nzaza na mrukukumbo nasikia Kuna mabilionea wa maparachichi nao tuone mashamba Yao.