Na Kabwamunyuma G Mhulo
Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa sasa ni Ndaisaba George Ruhoro aliyeshinda kwenye Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.
Uchaguzu huo ulikuwa wa kinyang’anyiro cha hali ya juu kwani watia niawalikuwa zaidi ya 40.
Ingawa Wilaya ya Ngara inaendelea kushuhudia mtililiko wa wanasiasa kutoka vyama mbali mbali wakija Wilayani kunadi vyama na sera zao pamoja na kuhimiza wananchi washiriki vyema kwenye uchaguzi wa mwaka 2025; wakazi wa Ngara wamekua wanataja baadhi ya wagomea wanaoweza kushiriki katika uchaguzi ujao.
Mapaka sasa, ikiwa bado miaka 2 ya kufanyika Uchaguzi mkuu wa 2025, tayari baadhi ya majina ya watu wanaotajwa kugombea yameanza kutajwa tajwa.
Hiisafari.com sio ya matumaini ila lazima ifanyike tuu. WanaNgara wanajadiri na kuona wale wanaofaa kuongoza wilaya ya Ngara. Iwe kwa miguu ama kwa ndege, Safirileo.com inatutosha na tuendelee kujadiliana ili tumpate yule ambaye anatufaa na kwa manufaa ya Ngara yetu.
Majina hayo ni pamoja na 1.Eng. Kakoko aliyrwahi kuwa Mkurugenzi wa Bandari,
2.Steven Kagaigai aliyekuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,3.Kijana wa mzee Nrukamazina ambaye Baba yake aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara,
3.Oliva Semuguruka ambaye ni Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Kagera,4.Issa Samma mtaalamu wa Siasa ambaye amewahi kugombea Ubunge na kuongoza mara nyingi kwenye Kura za maoni
Wengine ni
5.Dr. Philmoni Sengati aliyewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora,6.Lameck Kumbuka kijana wa Kabanga makini anayeishi Uswisi,
7.Bi.Hellena Adrian Ghozi mmiliki wa Shule katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ngara.
8. Alex Rafael Gashaza Mbunge msitaafu aliyeshindwa kutetea nafasi yake 2020 na kugaraazwa na Ndaisaba Ruhoro, pia wapo Vijana wawili ambao ni 9.Jimmy Nchunda na 10.Baraka Bitariho wote wanaishi Marekani.
Wengine wanaoonekana wanafaa ingawa hawajiishi mojabkwa moja ni pamoja na 11. Bw. Juventus Juvenary aliyeng’atuka kutoka katika kiti cha ukatibu wa Mbubge wa Ngara ili asogelee wananchi kwa ukaribu, 12. Bw/Mzee Sigaye ambaye alikua ni rubani na kanari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), 13. Angalau mtoto mmoja kutoka kwa mzee Majanja, 14. Na jina la ukoo wa Bahemu lilitajwa katika utafiti ulioganywa na gazeti hili.
Hata hivyo, idadi ya wagombea inaweza kuongezeka. www.simamia.com itaendelea kukufahamisha kuhusu maoni ya wananchi kuelekea Uchaguzi
Na baadae tutafanya Uchambuzi wa kila mgombea tukilinganisha na Utendaji kazi wa Mbunge aliyeko madarakani.
Recent Comments