Recent Comments

NGARA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KINAWEZEKANA

By Mwafrika Sep 5, 2023

NA ANKO G

Wilaya ya Ngara ni wilaya ambayo imebarikiwa kuwa mabondena mito mingi ambayo hutunza maji kipindi cha kiangazi lakini ni walaya ambayo mpaka sasa wakulima wengi wanategemea kilimo cha mvua hivyo inapo tokea uhaba wa mvua wakulima wengi wanaweza wasinufaike na kilimo.

Hata hivyo simamia.com imefika katika bonde la mto Goyagoya linalo patikana katika mamlaka ya mji mdogo Rulenge na kushuhudia shughuli mbalimbali za kilimo cha umwagiliaji zikifanyika katika bonde hilo huku shughuli hizo zikichukua eneo dogo linalo zunguka kingo za mto huo.

Vilevile simamia.com imebaini kuwa kilimo kinacho fanyika katika bonde hilo ni hatarishi kwa mazingira kwani wakulima hulima kwenye kingo za mto ambapo kipindi cha mvua husababisha mmomonyoko wa udongo unao pelekea uharibifu wa mazingira kwa kujaza udongo ndani ya mto ambapo husababisha kina cha mto huo kupungua na hata kukauka baada ya miaka kadhaa ijayo.

Pia simamia.com imashuhudia kilimo cha mahindi kikifanyika katika bonde hilo ambapo kwa mkilima anapata faida kubwa kwani kipindi cha kiangazi mahindi huuzwa bei kubwa ukilinganisha na kipindi cha mvua ambapo mahindi hupatikana kwa wingi hii inadhihirisha kilimo cha umwagiliaji kilivyo na faida kubwa.

Uzalishaji wa miti kama vile Mikaratusi, Parachichi n.k ikiwa ni moja wapo ya shughuli zinazo fanyika katika bonde hilo kwani katika kipindi cha kiangazi miti hiyo huoteshwa kwaajili ya kusubilia kupandikiza kipindi cha masika ama kipindi cha mvua.

Kilimo cha nyanya pia ni miongoni mwa shughuli zinzo fanyika katika bonde hilo ambapo wakulima hupanda nyanya hizo kwaajili ya matumizi ya biashara na matumizi ya nyumbani kutokana na ukubwa ya eneo analokuanamiliki mkulima.

Bonde hilo pia hutumika kulima mpunga hasa kipindi cha mvua nyingi kwasababu mpunga hihitaji maji ya kuchosha ili kupata mazao yaliyo bora na kwa wenyeji wa wilaya ya Ngara hulima mpunga wa asili ambao wao wanauita Mterano ni aina ya mpunga ambayo haitoi harufu kama ule mchele unaoitwa Super lakini wenyewe unasifa ya kuvimba pae unapopikwa.

Lakini pia simamia.com imeshuhudia kina cha mto Goyagoya kikipungua kila kukicha jambo ambalo ni hatari kwa mazingira nap engine kupelekea mto huo kutoweka kabisa kwa miaka 25 ijayo mpaka miaka hamsini endpo juhudi za kuunusuru mto huo zisipo chukuliwa.

Ni vyma kuzingatia kanuni za uhifadhi wa vyanzo vya mito na kufanya kilimo cha umwagiliaji cha kisasa kwa kutumia mitambo ambayo inaweza kuchota maji kutoka mtoni badala ya kumwagilia kwa kutumia mikono kama inavyo fanyika hivi sasa.

Mikoa kama Morogoro, Pwani, Dodoma,Singida n.k ni maeneo ambayo shughuli za kilimo cha umwagiliaji hutumia maji ya visima ama wanapo tumia maji ya mito basi hulazimika kufunga mitambo ya kuweza kufikisha maji shambani badala ya kulima kwenye vyanzo vya maji.

Serikali na wakulima wa wilaya ya ngara hili mlitazame kwa jicho la tatu kwani bonde la Goyagoya linawakilisha mabonde mengine mengi yanayo patikana wiaya ya Ngara ambapo simamia.com haijafika lakini ni vyema kutambua kuwa mito ni ya mhimu kuliko faida ndogo inayo patikana hivi sasa kutokana na kilimo kinachofanyika hivi sasa.