SERIKALI IINGILIE KATI MBEGU ZA MAHINDI NGARA
NA,ANKO G
Katika kipindi hiki cha Septemba katika wilaya ya Ngara tayari mvua zinanyesha na wakulima wengi wamesha lima mashamba yao huku wengine wakiendelea kupanda mazao mbalimbali hususa ni mahindi.
Hata hivyo suala la upatikanaji wa mbegu za mahindi imekua changamoto kubwa huku zikiadimika na kupanda bei.
Hata hivyo simamia.com imefika katika duka moja wapo la kilimo na mifugo ambapo bei ya mbegu aina ya SEED CO ikiuzwa kati ya Tsh 15,000 na Tsh 16,000 huku mbegu aina ya DELKAB ikiuzwa Tsh 20,000 kwa mfuko mdogo wa Kg2.
Aidha licha ya bei ya mbegu hizo kupanda bei ukilinganisha na bei za awali bado mbegu hizo hazipatikani hata kwani mbegu zinazo patikana ni chache ukilinganisha na uhiataji wa wawakulima.
Poa wakulima wengine hulazimika kupanda mbegu za asili kutokana na ukosefu wa mbegu za kisasa zinazo uzwa kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
Kilimo chenye tija huhitaji mbegu za kisasa ili kupata mazao mengi hivyo kukosekana kwa mbegu za kisasa inaweza pelekea kiwango cha uzalishaji katika msimu huu wa mwaka 2023/2024.
Ikumbukwe kuwa katika kipindi hiki cha mwezi Septemba na mwezi January wakulima wengi katika wilaya ya Ngara hupendelea kupata mazao ya mahindi kwasababu ni kipindi cha mvua nyingi pamoja na mazao mengine yanayo stahimili mvua nyingi huku mwezi Februari na mwezi Mei wakulima wengi wakulima zao la Maharage.
Serikali iingilie kati suala hili kwani wakulima wengi hulazimika kutumia mbegu hukotoa Burundi ambazo bado hazijathibitishwa kitaalamu nchini.
Recent Comments