Recent Comments

WAHITIMU WA DARASA LA SABA WAASWA KUENDELEA NA MASOMO.

By Mwafrika Sep 21, 2023

NA,ANKO G

Hamim Baruan mwanasiasa na mgeni rasimi katika mahahafali ya darasa la Saba shul ya msingi Kabanga awaasa wahitimu kujoandaa vyema na kuendelea na masomo ili kuiwakilisha vyema shule hiyo na kutumia vizuri kipindi cha kusubilia matokeo ya kidato cha kwanza.

Aidha hamimu amewataka wazi kuwaandaa vyema wanafunzi hao, kujiandaa kiuchumi na kisaikolojia kwaajili ya kuwatumizia mahitaji yao pale watakapo jiunga na kidato chakwanza.

Vilevile Hamimu amewaasa walimu kuendelea kuwalea vyema wanafunzi wanao endelea na masomo shuleni hapo kwa kushirikiano na wazizi ili kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza.

Hata hivyo Hamimu amewataka wazazi kuto zuia watoto kuendelea na masomo kwa kuwatumia kwenye shughuli za kilimo.

Pia Hamimu amepongeza waandaji wa sherehe ya wanafinzi hao kwa kuvaa mavazi ambayo yanaweza kutumika kidato chakwanza katika shule ya Sekondari Kabanga hii itapinguza gharama na inaashiria kuwa wanafunzi wote wanaweza kujiuna na elimu ya Sekondari.