Na mwafrika
Tanzania 🇹🇿 ni nchi iliyopatikana baada ya kuungana kwa nchi mbili (2)yaani Tanganyika na Zanzibar hapo ndio akazaliwa mama yetu Tanzania.
Kwa upande wa elimu leo naomba tupeane makalu live hapa bila kupepesa macho wala bila ya kumuonea aibu mtu na ni kwafaida yetu na Taifa letu vizazi kwa vizazi.
Elimu ya Tanzania(Tanganyika)ina mfumo wa tofauti na elimu ya Zanzibar,sasa naomba tuzungumze hii ya kwetu huku Tanganyika,mfumo wetu wa elimu ni kuanzia kindagate,shule ya msingi la kwanza mpaka la Saba,sekondari kidato cha kwanza mpaka cha 4 ba kisha kidato cha 5 na 6 kisha chuo.
Sasa humu kote kijana wa tz anajifunza mambo mbalimbali mpaka kufikia level ya chuo ndio anachagua kitu kimoja kwa mustakabali wa maisha yake ya baadae.
Ok that is not big deal ngoja tuje hapa kwenye namna ambavyo kijana akiwa chuoni huona maisha ni kama mteremko na hii ni kwa wengi wetu tuliosoma tulichukulia hivyo kwakua hatukuambiwa ukweli au muda mwingi tumekulia mashuleni na bila kujihusisha na shughuli za mitaani au hata kujifunza.
Hii imekua tabu sana na huanzia huko mavyuoni kwa walimu ambao wana elimu kubwa na ma PHD ya kutosha tu,hawa huwa wanafundisha watu wakimaliza waajiliwe na pia wengi hawahusiki na kuongea na wanafunzi wao ya kuwa maisha ya chuo sio maisha ya mtaani au kwa lugha nyepesi kuna maisha yanawqsubiri baada ya kutoka chuoni.
Huku mtaani ni pagumu sana wala sio utani hasa ikiwa unamawazo ya kuhitimu chuo/shule na kupata ajira moja kwa moja hapo utafeli maxima.
Hapo kitambo kidogo wengi walikua wanakimbilia ualimu na mambo ya utabibu kwakua ajira zilikua za uhakika jambo ambalo kwa sasa ni tofauti kabisa yaani kiufupi kila kona kumebana nganganga.
Siku hizi kila nyumba kuna Shahada au stashahada ama astashahada na hii yote ni kutokana na serikali kuhimiza watu kusoma na wakaitika hasa ila sasa baada ya wasomi kuwa wengi mchawi amekuwa ni kupata kazi imekua kazi.
Vijana wanakaribia kufanya mitihabi ya kidato cha nne na kuna wale waliohitimu lasaba wote hawa wanamalengo tofauti tofauti ila hapa niwashauri tu kuanzia wazazi/walezi na watoto kuwa Elimu haina mwisho ila maisha yana mwisho.
Vijana mkiwa shule jichanganyeni mitaani japo kuna hawa mabwenyenye ambao yoka vidudu mpaka chuo hajui jembe lipoje na chuo anasomea Kilimo daag Acha nincheke kidogo hahahaha,sasa siwadhihaki lakoni nawaonea huruma hebu msijifungie ndani mambo yamebadilika sasa sio kama zamani.
Ukiwa bado upo chuo jichabganye ili ukijitimu na kukosa kazi basi usiwe mzigo kwa mzazi kwa maana haiwezekani mzazi auze mifugo au mashamba ili usome kisha unamaliza unaanza kukaa nyumbani na kujaza ….ngoja nisimakize utamu ila naamini kuna kitu utakua umeelewa nikuombe angusha comments yako hapa chini.
Recent Comments