NA,ANKO G
Tunapo zungumzia ofisi tunazungumzia uwekezaji ambao hupelekea ajira na kutengeneza kipato kupitia uwekezaji huo huenda ni kazi za kutumia akili ama hata zile za kutumia nguvu.
Katika taifa la Tanzania wapo wawekezaji wa aina kama tatu amazo ni wakezaji wa ndani ambao wanaishi ndani ya nchi, Wawekezaji wageni kutoka mataifa mengine na wakwezaji waishi ughaibuni.
Wawekezaji wote hao wanapo wekeza huwa wanahitaji nguvu kazi kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za uwekezaji huo ambapo kupitia nguvu kazi hiyo hupewa ujira kutokana na uwekezaji huo.
Licha ya wawekezaji kuwaamini watu katika shughuli mbalimbali za ukwekezaji watu walio wengi wanapokua wanafanya kazi wanawaza kuwa uwekezaji huo siyo wakwao bali wanavyo fanya kazi wanamnufaisha muwekezaji.
Kutokana na fikra hizo walizo nazo watu wengi hupelekea kuhujumu uwekezaji huo na mwisho wake kupelekea uwekezaji kuendelea na hata kusimamisha Miradi wasabahu ya uhujumu unao fanyika.
Ukwekezaji nauchukulia kama mti wenye matawi unavyo kua huleta kivuli na matunda lakini unaweza kutengeneza mbolea kupitia kupukutisha majani na hata kuutumia kwa shughuli nyingine.
Uhujumu nauchukulia kama mtu kupanda kwenye tawi moja wapo kulikalia na kisha kulikata.
Kinacho tokea mtu huyo atadondoka na tawi hilo mpaka chini na kisha kuvunjikavunjika ambapo katika hali hiyo itakua ngumu kupanda tena lakini kudondoka kwake hakuzuii mti kuendelea kukua bali kutokana na ulemavu anao weza kuupata baada ya kudondoaka na tawi unaweza sababisha asiufaidi tena huo mti.
Kutoka na watu wengi kujawa na uhujumu wanafukuzwa katika ofisi ama wawekezaji kuhamisha ofini na kuwahamisha watu vitengo hilo ni sawa na mtu kudondoka na tawi.
Unapo aminiwa aminika ukipewa nafasi/ofisi chukulia ni kama umekabidhiwa mti umwagilie, upalilie na uutunze ili ukupe matunda na kivuli.
Hivyo kila mtu mtu atambue kuwa anapo pewa nafasi katika uwekezaji ama ofisi tambua kuwa ni ofisi au uwekezaji ni vyako kwani unaendesha maisha kupitia kazi hiyo ukiiharibu umejiharibia mwenyewe na siyo muwekezaji.
Recent Comments