Recent Comments

SERIKALI IINGILIE KATI UVUNAJI WA PARACHICHI NGARA.

By Mwafrika Oct 20, 2023
Hili ni rundo la Parachichi zilizoharibika kwa kukosa vigezo na kugeuzwa mbolea

SERIKALI IINGILIE KATI UVUNAJI WA PARACHICHI NGARA.

NA,ANKO G

Kilimo cha Parachichi wilayani Ngara ni kilimo kinacho inua uchumu wa wakulima kutokana na uuzaji wa zao hilo ndani na nje ya nchi.

Hili ni rundo la Parachichi zilizoharibika kwa kukosa vigezo na kugeuzwa mbolea
Hivyo nasi simamia.com imefika katika eneo la Nzaza kata ya Kabanga na kushuhudia parachichi aina ya HASS zinazo kadriwa kuwa kati ya tani 4 mpaka 5 zikiwa zimemwagwa pembezo mwa barabara zikidaiwa kukosa vigezo vya soko la zao hilo.

Vilevile inaelezwa kuwa parachichi hizo zaidi ya nusu zilivunwa zikiwa bado hazijakomaa hivyo kampuni zinazo jihusisha na ununuzi wa zao hilo kushindwa kuzinunua kutokana na kuto kidhi vigezo vya soko.

Parachichi aina ya Hass zaidi ya tani 3 zimetuowa kwa kukosa vigezo kabanga
Hata hivyo baadhi ya wakulima wamekua wakipata hasara kama hii kwa kuvuna parachichi kabla ya wakati wake jambo linalo pelekea kukosa mapato kwa mkulima na mapato ya serikali.

Pia serikali inapaswa kuweka sheria zinazo muongoza mkulima wa parachichi kuto vuna kabla ya wakati na hata kuweka misimu ya uvunaji kama wanavyo fanya Kenya ambapo kwasasa wamafunga uvunaji na ununuzi wa parachichi hasa aina hii ya HASS.

Kilimo cha Parachichi ni kilimo chenye tija katika wilaya ya Ngara na kilimo kilimo ambacho kimeinua wakulima wengi kiuchumi na kuchangia pato la wilaya.