Recent Comments

MFAHAMU PAUL MAKONDA KWENYE SIASA NA UONGOZI

By Mwafrika Oct 25, 2023

NA MWAFRIKA

Paul Christian Makonda amezaliwa tarehe 15/2/1982 katika mkoa wa Mwanza nchini Tanzania,Makonda ni mwanasiasa wa chama cha Mapinduzi [CCM].

Paul Makonda amesoma katika chuo cha ushirika Moshi pia amesoma chuo kikuu Mzumbe.

Alipata umaarufu katika kipindi cha Bunge la katiba ambapo alikua ni miongoni mwa watu wachache waliobahatika katika bunge hilo la kutunga katiba.

Makonda hakuishia hapo alipata umaarufu zaidi kwenye siasa na uongozi baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na baadae mwaka 2016 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam na Hayati JPM Rais wa awamu ya 5 wa Tanzania.

Akiwa Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam Makonda alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliosimama na jamii katika kutatua matatizo mbalimbali pia alipinga vikali matendo mahovu kama madawa ya kulevya na kudeal na watu wa mapenzi ya Jinsia moja.

Katika kipindi cha janga la Covid-19 makonda aliungana na aliyekuwa Rais hayati John Pombe Magufuli kuwahimiza watanzania kujikita kwenye maombi ili kuondokana na gonjwa la Corona na kiasi fulani watu waliamini.

Mnamo tarehe 31/1/2020 nchi ya marekani ilitoa tamko la kumzuia Makonda kuingia nchini Marekani kwa madam mbalimbali ikiwemo kuingilia vyama vya siasa,kunyima watu haki ya kuishi,kuua vyama vya upinzani na kukiuka haki za binaadamu.

Kitu pekee na kikubwa cha kumsifu Paul makonda ni miongoni mwa viongozi ambao wanapenda sana media na kutojali ukubwa ama udogo wa media,pia makonda ni miongoni mwa viongozi wanaopenda kuongelewa kila uchwao jambo ambalo kwa chama cha Mapinduzi kitakuwa kimeramba dume kwenye nafasi waliyomteua kuwa Katibu wa Nec Itikadi na uenezi Ccm Taifa.