Na mwafrika:
Huu ni ukweli mtupu nawaambia ndugu zangu maana hii Dunia lazima tujue mbichi na mbivu ili baadae tusiambizane hatuambiani ukweli wa mambo yalivyo.
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekua na wimbi la vijana ambao hawataki kuoa ama kuolewa kwa kudai wanakula ujana huku ili hali maisha yanasonga na umri unazidi kwenda mbele na haurudi nyuma.
Sasa nisikilize kwa umakini na soma kwa umakini namaanisha macho yako yawe makini usipepese wala usitazame pembeni kabisa,unajua piga hesabu tu mfano una miaka 30+ au 25+ na hausomi wala hakuna kimachokuzuia kuoa ama kuolewa.
Sasa kwanini usiingie kwenye majukumu ili hali umri unaruhusu na kipato kina ruhusu,hebu fikiria ukila bata au ujana uzeeni utakula nini sasa?badilisha mfumo wako wa maisha usiishiishi bali ishi kwa malengo na wakati.
Wakati haukusubiri na umri wako haukusubiri bali kila siku zinavyozidi kusonga mbele ndio na wewe unasonga mbele na kuukaribia uzee na kifo,huwezi kukwepa majukumu kwa kisingizio cha kula ujana acha ushamba badilika maisha na majukumu hayaogopwi.
Haya mfano una miaka 30 na haujazaa au haujazalisha kiufupi hauna mtoto na hushtuki tu bado,kwa mfano unataka upate watoto ukiwa na miaka 40 je hapo unazani watoto watakuita babu au baba?badilika acha kula bata mwili wako na Dunia visikuchanganye haya ni mapito tu.
Hongera kwa watu wa vijijini maana maana %kubwa wanaoa ama kuolewa wakiwa bado vijana wenye nguvu zao,Asante kwa kusoma endelea kutufuatilia simamia.com kwa habari mbalimbali na ushauri.
Recent Comments