Recent Comments

BAISKELI YA POLISI KATA YAFIKA KILABU YA POMBE ZA KIENYEJI – IGOMBATI.

By Mwafrika Nov 6, 2023

Morogoro.

Kwa kutumia usafiri wa Baiskeli Polisi Kata wa Kata ya Lumemo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/Insp) Edwin Kipimo amekuwa akitembelea makundi mbalimbali ya watu kwa lengo la kutoa elimu ya Polisi Jamii.

Aidha, Novemba 6, 2023 Mkaguzi Kipimo amefika kwenye Kilabu ya Pombe ya kienyeji na kuzungumza na Wazee waliokusanyika eneo hilo kwa lengo la kupata mvinyo.

Katika Kilabu hiyo, Mkaguzi Kipimo aliwataka wananchi hao wanywe vilevi hivyo kwa kipimo ambacho hakitaathiri utimamu wa akili na mwili kuepuka kutofanya maamuzi sahihi, kuepuka kudhalilika na kuwa kituko kwa jamii.

Vilevile, aliwaasa wazee hao kurudi nyumbani mapema ili kuzungumza na familia zao hasa watoto kujua changamoto zinazowakabili na kuzitolea ufumbuzi.

Aidha Mkaguzi Kipimo ametembelea kijiwe cha Pool Table na kuongea na vijana kuhusu, kuepuka matumizi ya dawa za kulevya, kujiepusha na vitendo vya wizi na kamari na kutumia muda mwingi kufanya shughuli halali za kuwaingizia kipato na sio kukaa kijiweni na kumalizia safari yake ya kutoa elimu kwa watoto wa shule ya awali Lumemo.