Recent Comments

NGARA YAIFUKUZA NJAA VIKALI.

By Mwafrika Dec 15, 2023
Picha ya mti wa Parachichi

NA,ANKO G

Wilaya ya Ngara ni miongoni mwa wailaya za mkoa wa Kagera ambayo asilimia kubwa ya wakazi wake wanajishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali kama vile;. Mahindi,Maharage,Migomba, Parachichi n.k.

Picha ya mti wa Parachichi
Kutokana na mwaka uliopita mvua kuwa chache imepelekea bei ya vyakula kupanda bei ambapo kwasasa Kg1 ya unga wa mahindi ni Tsh1,500 kwa ambao haujakobolewa na Tsh2,000 bei ambazo zinaonekana kuwa kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.

Vilevile maharage yanauzwa kati ya Tsh1,500 mchanganyiko na TSh2,000 kwa maharage ya njano kwa bei za rejereja madukani.

Katika msimu huu mvua zinaonekana kuwa nyingi kuliko msimu uliopita hivyo simamia.com imepita katika baadhi ya maeneo na kushuhudia zao la mahindi likiwa limestawi zaidi kuliko msimu uliopita.

Kutokana na zao la mahindi kustawi katika sehemu kubwa ya Ngara kuna uwezekano mkubwa wa bei ya unga kushuka bei.

Lakini pia simamia.com imebaini kuwa zao la maharage limeathirika kutokana na mvua hizo kuwa nyingi kwani zao hilo halihitaji mvua nyingi, mvua zinapokua nyingi zinapelekea maharage kupatwa na hali ya kuungua na kupata mazao kidogo kama ilivyo tarajiwa.

Hata hivyo kutokana na Ngara kuwa na misimu ya kupanda maharage inayogawanyika mara mbili liko tumaini kwa msimu wapili wa maharage kupata maharage mengi zaidi kuliko msimu huu wa awali.

Pia kwa upande wa mazao mengine kama vile parachichi,Migomba na miti inaonekana kustawi kwasababu mazao hayo yanahitaji mvua za kutosha.