Na mwafrika
Katika kipindi hiki cha sikukuu kuna mambo mengi sana hutokea na hayo mambo uhusishwa na ushirikina,freemason na uchawi kiujumla lakini ukweli ni kwamba kila msimu wa sikukuu na mwisho wa mwaka msongamano wa vyombo vya moto huwa vingi barabarani na kila mmoja na udereva wake.
Kuna watu ambao ikifika kipindi cha sikukuu kama hizi za Xmass na mwaka mpya basi hukimbilia makwao kwenda kujumuika na familia/ndugu jamaa au watu wa karibu ili kufurahia kwa pamoja.
Yes sio jambo baya bali ubaya unakuja kwamba kwenye msafara wa mamba na Kenge wapo hapa namaanisha kuna ambao wametoka kununua magari mapya na wanataka kwenda kuonesha nyumbani sasa shida inakuja kwenye udereva yaani myu kanunua gari na kajifunza wiki tayari anaingia Road na safari kubwa anaendesha hapa lazima tuseme kuna kafara au ychawi wakati ukweli ni kwamba umakini na udereva wa baadhi ya wasafiri hauko sawa.
Hapa sisemi msiende makwenu no bali nawatahadhalisha tu kama una gari lako na hauna uhakika wa udereva wako basi kodi mtu mzuri aendeshe mpaka kwenu au kama ngumu bora upande mabasi tu ili kuepusha matatizo maana baada ya kisheherekea watu wengi msimu huu hulia.
Pia kuna hawa bodaboda[waendesha pikipiki]yaani mtu safari yake fupi ila sasa anapangua giant mpaka 4 sasa zanini wakati unapoenda ni chini ya kilomita 10?unawahi wapi wakati maisha yako ni bora sana kuliko haraka zako?
Pia kuna watu wanakodi gari ndogo haswaq baada ya nauli kupanda na gari kua chache kutokana na wingi wa watu sasa shida sio kukodi shida ni baadhi ya madereva waendeshao hayo magari mhh wengi sio wazoefu wa safari ndefu bali wengi wanaangalia pesa iliyopo mbele.
Nashauri vyombo vya ulinzi na usalama barabarani kuweni makini na wasafiri na hasa kuna hawa wenye private cars daah hawa watu wanawahi sana yaani mtu anatembea usiku speed 120 utazani hana roho jamani tuepuke haya lakini pia nishauri tu kama sio lazima kusafiri baki nyumbani ma familia yako ili kuepusha mosngamano na sikukuu zikiisha utaenda kwa utaratibu mzuri tu.
Mwafrica kazi nzuri,
Ni kweli katika kipindi cha sikuu Kama hizo huwa kunakuwa na hatari kubwa juu ya maisha ya watu, ambapo kila uasi, uharifu na Mambo mengine hutoka sana.
Hasa, katika kugharimu maisha ya wanadamu ndugu kupoteza watu wao, wengine kupoteza mali wakijua wanaokoa
Ni Mambo kadha wa kadha ambayo ni hatarishi sana
Ahsantee,
@ciptschannel2024 kwa viwango vingine#
Mwafrica kazi nzuri,
Ni kweli katika kipindi cha sikuu Kama hizo huwa kunakuwa na hatari kubwa juu ya maisha ya watu, ambapo kila uasi, uharifu na Mambo mengine hutoka sana.
Hasa, katika kugharimu maisha ya wanadamu ndugu kupoteza watu wao, wengine kupoteza mali wakijua wanaokoa
Ni Mambo kadha wa kadha ambayo ni hatarishi sana
Ahsantee,
@ciptschannel2024 kwa viwango vingine#