Yawezekana kwa wengine, hii ni hitimisho la kwanza katika safari ya kusaka elimu ya juu, pengine kwa wengine wametia nukta katika elimu na kuungana na soko la kazi. Pengine hizi mbio zimefikisha wengine ambapo sasa watategemea wapandishwe vyeo huko wanapobadilisha muda wao kwa mshahara wa kila mwezi.
Kwa hali yoyote, wahitimu wanastahili pongezi kwani safari ya kutafuta usomi sio nyepesi.
Hawa ni baba, mama, wake, waume, makaka, ama madada ambao wakiwa kwenye harati za kutafuta vyeti vya nyanja mbali mbali, hawakuweka pembeni wajibu wao katika jamiii. Na leo kwa kuwa wamekuwa kioo chema kwa wengi wetu na nguzo bora kwa Ngara, na kwingineko watakapoishia baada ya kuhitimisha masomo yao, their futre is lighten up!
Pongezi nyingi ziwafikie uongozi na wafanyakazi wote waliopo pale Moonshine Training Institute kwa kuwawekea mazingira bora ya kielimu. Pia hongera kwa hiki chuo kwa kuwa na campus mpya iliyopo Kasulo K9 Lukole na kwa kuona shughuli ya mahafali ya mwaka 2023 inaenda vizuri hususani kwenye campus mpya. Kama picha zinavyoonyesha, kazi haikuwa nyepesi ila imemalizika vizuri.
Recent Comments