Recent Comments

Mbunge Kudhani Pesa Ndio Kila Kitu Huo Ni Uzwazwa

By Baraka Bitariho Dec 20, 2023
Ndugu zangu Wana Ngara ambao hamkufanikiwa kufika nyumbani kwaajili ya mapumziko ya Sikukuu za Noeli na Mwaka mshasha mmekosa uhondo!
Kuna mambo ya ajabu yanaendelea sikuwaho kuyaona Katika maisha yangu yote Duniani takribani miaka 60 na usheee!
Dhana ya Utawala Bora tusiitegemee wala MAENDELEO yenye uwajibikaji thabiti kutoka kwa Mbunge aliyepo kwa Sasa
Kinachoendelea  jimboni ni kufuru na udharirishaji wa Wananchi. Haluchaguliwa ili Kuja kuwalipa Pesa,alichaguliwa kuisimamia Serikali kutimiza wajibu na kuharakisha MAENDELEO. MBUNGE ameligeuza Jimbo kuwa Bustani ya Wanyama, au zizi la kulishika mifugo kwa kuwahonga Pesa na kujitafutia Ushawishi tu!!! Hii ni aibu na tutachekwa daima.
Nimesoma chapisho mtandao wa Jamii Forums, naomba kushirikisha hapa. Tusome na tulinganishe na Hali halisi jimboni Ngara huku tukiviomba vyombo husika kumulika Ngara.
TAKUKURU,TUME YA UCHAGUZI na Chama tawala tafadhali fikeni Ngara.  Na kama mpo, basi amkeni wasaidie Watanzania wenzenu
Log in
 Habari na Hoja mchanganyiko
Pesa ndio kila kitu kweli?
 Thread startermende 2014
 Start dateMay 6, 2014
mende 2014
JF-Expert Member
May 6, 2014
#1
“Wapo wanaodai” “PESA NDIO KILA KITU” SI KWELI!,” PESA SIO KILA KITU” ‘Pesa yaweza kununua (KITANDA) wala sio (USINGIZI),
Pesa yaweza kununua (SAA) wala sio (WAKATI),
Pesa yaweza kununua (KITABU) wala sio (MAARIFA),
Pesa yaweza knunua (CHEO) wala sio (HESHIMA),
Pesa yaweza kununua (DAWA) wala sio (AFYA),
Pesa yaweza kununua (DAMU) wala sio (UHAI),
Pesa yaweza kununua (ANASA) wala sio (UPENDO),
Pesa yaweza kukupeleka (INDIA NA CHINA) wala sio (MBINGUNI) umeamini kuwa pesa sio kila kitu au unakataaa? Mheshimu Mungu yeye ndio kila kitu sio pesa
Ushauri kwa Mbunge wangu,Kijana Bado una uwezo wa kukimbia na kutafuta. Hakuna haja ya matumizi makubwa ya Pesa kushawishi na kulaghai watu.
Kama unapendwa, utachaguliwa. Ila, usishawishi na usitumie Pesa hivyo. Acha dharau