Huyu ni mbunge ama Rais wa Nchi, pengine huyu ni katibu wa Idara fulani. Hii ni picha tuu na kama nyota yake haijang’aa vizuri, huyu ni mtu wa kawaida tuu anayeendesha boda boda ama muuza bidhaa ndogo ndogo maarufu kama mmachinga.
Baada ya kutoka Shule na kutokana na mazingira aliyokulia na kusomea, mwanzo wa maisha yake yalikua hayatamaniki. Ndio kama jiwe alilipata tena kutoka kwenye shule nzuri tuu. Kazi zaina zote ni kama alizifanya na baada ya muda nyota yake ilianza kung’ara. Hadi nafasi za siasa alizitafuta na kutokana na historia ya Ukoo wake, hakubatika kuibuka mshindi kwenye chaguzi.
Kama waswahili wanavyosema, penye Nia pana njia, kwenye kampeni zake, ilikua wazi hakupoteza imani na tumaini kuwa ipo siku atavuna matunda kutoka kwenye harakati za kisiasa. Kama mwanasiasa chipukizi, ahadi nyingi tuu aliziahidi na kati ya aliyoyatamani kuyatimiza atakapochaguliwa ilikua ni kuboresha huduma za afya, elimu, na upatikanaji wa vyakula vya kutosha pamoja na kuboresha bara bara na njia za uchukuaji kwenye jimbo lake.
Mungu hujibu sala kwa wakati wake na muda mwingine majibu ya sala yanakuja muda tofauti na uliotegemewa na muombaji. Kipindi fulani basi upepo ulivuma vibaya na watangaza nia walikuwa wengi na kama ilivyo ugomvi wa panzi ni faida kwa kunguru. (Wahenga walisema Vita vya Panzi ni Furaha kwa Kunguru) Kutokana na uzito wa mashindano kwenye kampeni, jamii ikaona ni bora imchague mwanasiasa ambaye alikua anatoa jumbe zenye ahadi zitakazoleta nuru na amani kwenye jamii. Huyu ndie ameibuka mshindi kwenye uchaguzi kwaajili ya kuwakilisha jimbo lake.
Wapinzani wake walipoteza muda kugombana na kurushiana maneno kwenye kampeni, hali iliyopelekea jamii kuwaona hawafai. Mmoja wa mpinzani alijitutumua na kudai kuwa kutokana na uwepo wake kwenye siasa, anauzoefu sana kisiasa, amekusanya na kushiba na hayupo kwenye hili nyang’anyiro kutokana na njaa kama wapinzani wake. Na uzoefu wake kwenye ulingo wa siasa, alipigwa chini na huyu ambaye haijulikani kama ataleta huduma bora ya afya kwa familia yake, ataboresha shule ambayo iliwapiga teke ndugu na ukoo wake, ama sasa ataenda kujenga bara bara ambayo haifiki hata nyumbani kwake.
Pengine atakua kama baba yake na kuzaa watoto wengi ambao kesho yao ni giza nene. Watoto wengi ambao hawana elimu ama mafanikio kimaisha wanageuka kuwa mzigo kwa jamii. Na mmoja wapo anapofanikiwa kuwa nguzo kwenye ukoo, basi anapaswa asaidie ndugu zake.
………..
Sasa mwanasiasa anapoweka ahadi ambazo masikioni mwa wapiga kura zinasikika kuwa ni nzuri na kuonekana kuwa zitaleta maboresho mema, kitendawili kinachobaki ni kama hayo maboresho yataletwa kwenye familia yake ama lah? Utatoaje afya bora ambayo hukubahatika kuwa nayo, elimu ambayo ulipunyuka punyuka na kuwaacha ndugu zako waking’aa macho tuu. Ama mafaniko ya Huyu ndio msalaba mzito amebahatika kuubeba kwa niaba ya ukoo na jamii yake?
Kiongozi mzuri ni yule anayejiangalia na kutathimini mienenendo yake. Mienendo ya maisha yake ya binafsi na maamuzi mema ya kile anachoongoza. Kama ataamua kujaza watoto wake bila mpangilio, ataweza vipi kutimiza ahadi aliyoitoa kwa mpiga kura eti ataboresha huduma ya elimu? Atajenga madarasa ambayo ndugu zake hawatoingia ama vituo vya siasa ambavyo yeye mwenyewe atakimbia na kuelekea ulaya kwa vituo vilivyojengwa na mwanasiasa mwingine? Kuzaa watoto wengi kwa kiongozi ni ishara ya kiburi cha pesa ambazo hazitokuwepo watoto wake wakishakua. Hata kama zitakuwepo, hazitotosha idadi ya watoto wake na kupelekea hali halisi kama inavyoonekana kwenye hiyo picha; mmoja wa watoto kuponyoka na kufanikiwa kishule ama kimaisha ambapo jamii inaishia kujiuliza kama haya ni mafanikio ama ni msalaba mzito utakaobebwa na nguzo moja kama inavyoonekana pichani.
Ni bora tuzae kwa mpango na kwa malengo kwani kesho yetu hatuijui. Ni vizuri watoto wachache katika familia wainuke na kuwa nguzo ili uzito wa kusaidia wale ambao hawakubahatika kufanikiwa usiwe mzito. Haya malengo yote yatategemewa na kuchunga maisha yetu binafsi la sivyo utafanikiwa na ushundwe kupiga hatua za kimaendeleo kwani kama sio kutelekeza watoto wako, basi utajikuta upo nyumbani unalea watoto wako.
Ukiwa na watoto wengi ambao baadhi yao wametelekezwa, hutomshawishi mtu anayejielewa eti upigiwe kura kwani ukishinda utaleta maendeleo kwa wengine, maendeleo ambayo umeshindwa kuletea familia yako.utajengaje shule huku hujui utasomeshaje mwanao? Wale waliotelekezwa mitaani ni chanzo cha manung’uniko na pengine maisha yao hayana utoafuti na hao wanaoonekana pichani?
Kwa hiyo, tukiazima kiyovu, tunashauliwa let’s lead by an example kwani uongozi kwa mfumo wa remote control utaboresha umasikini na mazingira mabovu ya jimbo uliloahidi kuliboresha. Kwa jamii, huyu ni tegemezi pichani tuu na pengine atashindwa kuwa mkombozi wa familia na watoto wake kutokana na kushindwa kusimamia maisha yake binafsi. Kugawa pesa ni kununua watu, pesa zitakapokatika hizi sifa zitageuzwa kuwa matusi. Maendeleo yakukiwepo yataonekana tuu na yataongelewa jila hata kuhonga yule anayeyaona.
Huyu pengine ni mtoto wa kwanza, wa kati hama hata wa mwisho. Pengine Huyu ni wewe msomaji wa hii makala. La maana unakumbatia umaskini kwa kukumbatia uoga kwa kushindwa kufanya maamuzi bora kwa jamii? Huu uoga na tabia ya kuoneana aibu ndio huzalisha familia ambapo mmoja wao ndio hufanikiwa sana kuliko wengine na mafanikio kugeuka na kuwa msalaba mzito. Uchovu na manung’uniko havikosekani pale mmoja kati ya famila kubwa huwa ndie anaonekana kama kafanikiwa wakati moyoni anatamani hata huu msalaba angeepukana nao. Kama Huyu ni wewe, basi leo fanya maamuzi mema ili kizazi kijacho kisije kujikuta kwenye hali halisi inayoonekana katika picha zilizotumiwa kwenye makala hii.
Comments zenu chini ya hii makala ni muhimu katika kutengeneza kesho yenye nuru na neema.
Recent Comments