Pengine Jumbe toka kwa Rais wa zamini wa Zimbabwe, hayati Robert Mugabe zinaweza kugusa kila mtu popote alipo, awe mjini ama kijijini. Simamia.com na Ngaratv.com ikaonekana ni vyema zifike kwa walengwa.
Kumpongeza Mwanasiasa kwa kujenga Shule,Hospitali au Barabara kwa fedha za Umma ni sawa na kuishukuru Mashine ya ATB pale unapokwenda Benki kutoa Pesa. Hii Haina tofauti na kile kinachoshuhudiwa na Wana Ngara kumpongeza na kufagilia kwa Wanasiasa wanaowapa fedha kwa lengo la kutafuta Umaarufu na uungwaji mkono ili wawachague tena. WANANCHI wanatakiwa kutambua kuwa Pesa wanazopewa, mgoligoli na Gwagwa wanazonunuliwa ni Mshahara wao. Kuelekea Uchaguzi,Pesa zikija pigeni ila mjue kuwa ukichaguwa vibaya malipo yake ni Miaka mitano tena mpaka Uchaguzi. Dawa ya Malaria ni chungu ila inaponya. Baadhi ya Wanasiasa hawapemdi kuambiwa Ukweli,wafike sehemu wawaambie ukweli Wananchi. Tafakari, Chukua na hatua.
Recent Comments