Recent Comments

WALIMU WA SEKOMDARI WANAVYO IBIA WAZAZI NA WALEZI.

By Mwafrika Jan 4, 2024

NA, MWANDISHI WETU.

Ikiwa TAMISEMI wametuma ujumbe huu “Elimu ya sekondari humuandaa mtoto kukabiliana na changamoto za maisha. Hakikisha mtoto anaripoti shuleni kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.” kwenye namba za simu za baadhi ya wazazi na walezi inaonesha serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inahamasisha suala la Elimu katika mwaka huu wa 2024 hasa ngazi ya sekomdari.

Wakati hayo ya kuendelea na wazazi wakijipanga vyema kupeleka watoto wao mashuleni ni wakati ambao pia wazazi au walezi hao wanaibiwa na walimu kwa kujua ama kuto kujua hivyo basi simamia.com leo unaweka wazi wizi unao fanywa na baadhi ya shule za sekomdari nchini.

Aidha simamia.com imenaribu kupitia fomu za kujiunga na kidato cha kwanza katika shele X zinazo patikana wilayani Ngara ambazo zimeainisha mahitaji ya mwanafunzi anayo takiwa kufika nayo anapo jiunga na kidato cha kwanza na kubaini yafuatayo;

Fedha ya matibabu, fedha hii hutolewa kwa leongo la mtoto anapo uguo kuweza kutibiwa lakini watoto wanapo ugua hupewa vidonge vya kutuliza mauvu na anapo zidiwa hufukishwa katika vituko vya afya au kuruhusiwa kwenda nyumbani ambapo hutibiwa kwa gharama za wazazi hata kama ni magonjwa ambayo yangewezeza kutibiwa na na pesa iliyo tolewa shuleni hapo kama ilivyo kwenye shule za watu binafsi je pesa hiyo huwa inaenda wapi?

Pesa kwaajili ya dawati kila mwanafunzi anapo fika shuleni kujiunga na kidato cha kwanza hutoa pesa hiyo lakini chaajabu Bado shule zinalalamika kuwa hazina madawati ya kutosha licha ya mwanafunzi anapo hitimu kidato cha nne haondoko na kiti/dawati lake licha ya kuwa kuna baadhi ya wafadhili huwa wanafadhili madawati na mzazi hata akiwa na watoto wanao jiunga kidato cha kwanza kwa Miaka tofauti hawezi tumia dawati la alie tangulia. Lakini pia hata dawati likiaharibika mwanafunzi hutakiwa kulipa pesa na siyo dawati anapo hitaji kununua dawati alete shuleni huambiwa shule inaagiza kwa watengenezaji walio thibitishwa hutakiwa kutoa pesa na siyo dawati je, madawati ama vitu huwa vinaenda wapi?

Pesa ya uchakavu hii ni pesa ambayo humlinda mtoto anapo haribu kitu itumike kukinunua lakini mwanafunzi anapo haribu kitu ama kupoteza Mali ya shule hutakiwa kulipa pesa nje ya pesa ya uchakavu je, pesa hiyo huwa unafanya kazi gani?

Karatasi za kuandikia (Lim Paper) hizi karatasi wanafunzi hutakiwa kufika nazo wanapo jiunga na shule na hata baadhi ya shule huwa kila mwaka wanapeleka Lim peper lakini matumizi na idadi ya karatasi yanatia mashaka huku baadhi ya wadau wakiniambia simamia.com kuwa huwa kuna mchezo wa baadhi ya walimu kuuza limu hizo kwa wafanya biashara wa stationary.

Vifaa vya usafi kama vile; Fagio,Jembe,Ndoo, Fyekeo n.k katika baadhi ya shule mwanafunzi anajiunga kidato cha kwanza akiwa navyo lakini cha ajabu anapo hitimu anaviacha shuleni je huwa vinapotelea wapi?

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo baadhi ya wazazi na walezi wanajiuliza bila kupata majibu sahihi mengine yanayo husiana na kujiunga na Elimu ya sekomdari tutakuletea kwneye makala ifuatayo, Lakini sisi kama simamia.com tunatamani kama kuna mtaalamu anae weza kutwambia kwanini haya yanatokea atuandikie kwneye comment.

Ipo haja ya wahusika kuangalia hili na jinsi ya kuliwela sawa katika kutimiza sera ya Elimu bure nchini Tanzania.