NA, ANKO G.
Ukiondoa zao la Parachichi,Ndizi,Kahawa na mahindi wilayani Ngara Maharage ni miongoni mwa zao la kibiashara kwa soko la ndani na soko la nje ya wilaya hiyo.
Hata hivyo wilaya ya Ngara imebarikiwa misimu miwili mikubwa ya kilimo huku msimu wakwanza wa Septemba-Januari zikishuhudiwa mvua nyingi ambazo limepelekea athari kwenye mazao yasiyo hitaji mvua nyingi kama vile maharage na wakulima kujikuta wakipata hasara kwenye zao hilo.
Kuelekea Februari simamia.com imepita katika maeneo kadhaa wa kadhaa na kishuhudia wakulima wakiendelea kuandaa mashamba yao kwaajili ya kupanda maharage msimu walipi wa Februari-Mei.
Hata hivyo msimu huu wakulima wengi wameweka matarajio makubwa ya kuvuna maharage kwa wingi tofauti na msimu ambao unamalizika hivi sasa.
Vilevile ni utamaduni wa wakulima wengi wilayani humo kuamini kuwa msimu wapili ni msimu sahihi kwa zao la maharage licha ya kuendelea kuhushuhudia mvua nyingi kwa kipindi hiki.
Pia mborea na pembejeo nyingi za kilimo zimekua kikwazo kwa mkulima wa Ngara huku wakiendelea kupata pembejeo kwa bei kubwa ama kutumia pembejeo kutoka nchi jirani na walio wengi kulazimika kutumia mbolea zitokanazo na wanyama.
Hivyo basi simamia.com inaendelea kumfuatilia kila kinacho endelea na kukuletea kinacho kufaa katika ukweli na uhakika.
Recent Comments