Recent Comments

UKOSEFU WA MADAWATI NGARA WANAFUNZI WANAKAA CHINI.

By Simamia Ngara Feb 28, 2024

NA,MWANDISHI WETU.

Wakati serikali ikiendelea na utoaji wa elimu bure nchini Tanzania kuna baadhi ya shule wilayani Ngara mkoani Kagera zinakabiriwa na changamoto ya madawati na kupelekea wanafunzi kukaa chini wawapo darasani wakiendelea na masomo yao.

Aidha simamia.com imepita katika baadhi ya shule (Sekondari na Msingi) ambazo majina ya shule hizo yamehifadhiwa kwenye maktaba ya simamia.com na kushuhudia baadhi ya wanafunzi wakipata elimu yao huku wakiwa wamekaa kwenye sakafu.

Hata hivyo serikali imeweka viongozi wa kuratibu elimu katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata, ngazi ya wilaya,mkoa na hata taifa, hivyo basi viongozi wa wilaya ya Ngara fikeni katika shule husika kama bado hamna taarifa hizo ili mjionee watoto wanavyo soma kwa tabu.

Vilevile baadhi ya shule zinaendelea kuchangisha michango kwaajili ya madawati kutoka kwa wazazi pamoja na taasisi mbalimbali.

Pia simamia.com tumetoa taarifa hii ili viongozi kuweza kufika katika shule husika na kutafuta namna ya kutatua changamoto hii, kama halitafanyiwa kazi tutaandika habari nyingine ikiambatanishwa na majina ya shule zenye changamoto hiyo pamoja na picha za wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwneye sakafu.