NA,ANKO G.
Barabara ni moja ya mawasiliano katika jamii, Wakazi wa Kijiji cha Mrukukumbo ya chini Kata ya Kabanga iliyopo Wilayani Ngara mkoani Kagera wanakosa mawasiliano ya barabara inayo anzia shule ya msingi Murukukumbo mpaka kanisa la Sabato Mundimanga kwa miaka kadhaa sasa.
Aidha barabara hiyo ilitengenezwa na TASAF kwa zaidi ya miaka mitano iliyo pita na inaelezwa kuwa tangu barabara hiyo itengenezwe haijawahi kurekebishwa tena mpaka hivi sasa.
Hata hivyo barabara hiyo Ina mashimo makubwa na kipindi inatengenezwa haikuwekewa mitaro ya kupitisha maji jambo linalo pelekea maji kupita katikati ya barbara na kuifanya kuchimbika na kuwa kama mtaro wa kupitisha maji.
Pia asilimia 99% ya wakazi wa Murukukumbo ya chini ni wakulima hivyo barabara ni kero na changamoto kwa wakazi hao kwani hupata shida kupitisha mazao yao wanapo hitaji kuyauza na inapotokea wakayapitisha hulazimika kutumia gharama kubwa kwa kupandisha kwenye baiskeli au kutumia wanao beba kwa kutumia kichwa.
Hivyo basi wa kazi wa eneo hilo wameiomba serikali kuwakumbuka kwakua hata wao ni miongoni mwa wachangia kodi katika taifa la Tanzania.
Recent Comments