Recent Comments

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA MTANDAO WA FACEBOOK

By Simamia Ngara Feb 28, 2024

NA,ANKO G

Hivi karibuni kumeibika watu wanatumia mtandao wa Facebook kutapeli watu ambao hutuma link (Kiungo) kwa kutumia taasisi ya UNICEF na kumtaka mtumiaji wa mtandao huo kubofya link hiyo kisha kutakiwa kufauata maelekezo wanayo mpa ikiwemo kulipia kiasi fulani cha fedha na kisha kupokea pesa kiasi cha Tsh 2,464,000 ambapo mtumiaji huyo anapo fanya hivyo hutapeliwa na kuto pata kiasi hicho alicho ahidiwa.

Aidha watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapaswa kuwa makini pale wanapo tumiwa link (Kiungo) kwani kufanya hivyo hipelekea wengi wao kutapeliwa.

Vilevile ni vyema mtumiaji wa mitandao ya kijamii kuuliza watu wengine kabla ya kufuata maelekezo wanayo pewa katika mitandao hivyo.