Recent Comments

KUFUNGA IMEKUA UTAMADUNI WENGI HUSHINDA NJAA.

By Simamia Ngara Mar 29, 2024

NA,ANKO G.

Tumezoea kusikia mfungo kwa wakristo huita Kwarezima siku 40 na kwa waisilam mwezi mtukufu wa Ramandhani siku 30 ambapo waumini hufunga/kijinyima kula,kunywa na mambo mengine yanayo ufurahisha mwili kwa kusali na kumkaribia mwenyezi Mungu.

Aidha nichukue nafasi hii kuwapongeza wakristo kwa kuhitimisha funga hiyo ya siku 40 na kwa waislam Mungu awatie nguvu katika siku zilizo salia kuhitimisha funga yenu.

Hata hivyo kufunga kwasasa imekua utamaduni licha ya mafundisho na maandiko kuelekeza namna nzuri ya kufunga wengi wao hufunga kinyume na maandiko ama mafundisho kwani hushinda njaa jambo linalo weza kusababisha maradhi yasababishwayo na njaa.

Vilevile umekua utamaduni kwa walio wengi kufunga kwa kuafuata ratiba iliyo wekwa na dhehebu ama dini husika kwa kuwasindikiza walio fungu na badala yake kumnafikia Mungu ambapo hujizuia kufanya yale yaliyo katazwa huku wakipania kuwa baada ya kipindi cha mfungo kukamilika basi watalipiza kufanya yale yote ambayo hawakuyafanya kipindi cha mfungo na siku yakwanza tu katika kusherehekea kuhitimisha mfungo pasaka na Eid basi hufanya tena yale yote ambayo hawakuyafanya kipindi cha mfungo.

Kufanya hivyo ni kukiuka maandiko kwani mwenyezi Mungu anawataka waumini kufanya yaliyo mema hata kipindi ambacho siyo cha mfungo.

Waumini wanatakiwa kutambua kuwa maisha wanayo ishi kipindi cha mfungo ndiyo maisha wanapaswa kuyaishi hata katika kipindi kisicho na mfungo na hata kutafuta muda wa kufunga wakati wowote bila kujali kipindi cha siku 40 kwa wakristo na siku 30 kwa waisalam.